Wizara
ya Maliasili na Utalii imechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi wake
tisa (9) kufuatia kadhia ya utoroshaji wa Wanyamapori Hai katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na masuala mengine
yanayohusu Wanyamapori. Watumishi hao wamechukuliwa hatua husika
kufuatia kukamilika kwa uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikiwakabili.
(i)
Bw. Obeid F. Mbangwa -
Mkurugenzi wa Wanyamapori. Wakati wa kadhia hiyo alikuwa Mkurugenzi
Msaidizi Matumizi ya Wanyamapori,
(ii) Bw. Simon Charles Gwera – Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha,
(iii) Bw Frank Mremi - Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii – CITES na Utalii wa Picha Arusha.
(2)
Aliyeondolewa Cheo cha Madaraka kutokana na kutochukua hatua kamilifu
za ulinzi ambazo zingeweza kuzuia kutokea kwa tukio la utoroshwaji wa
wanyama ni:
(i)
Bw. Bonaventura M.C. Midala – Mkurugenzi Msaidizi,
Undelezaji Wanyamapori. Wakati wa tukio alikuwa Mkurugenzi Msaidizi
Sehemu ya Kuzuia Ujangili.
(3)
Wafuatao ni Maafisa Wanyamapori Daraja la II waliotekeleza maelekezo
ya Wakuu wao wa kazi yaliyo kinyume cha Sheria ambao wamepewa Onyo Kali
la Maandishi:
(i)
Bibi Martha P. Msemo - Afisa
Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Arusha.
(ii) Bibi Anthonia Anthony – Afisa Leseni, Ofisi ya Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha Dar es Salaam.
(4)
Bw. Silvanus Atete Okudo ni Mkuu wa Kituo cha Uwindaji wa Kitalii,
CITES na Utalii wa Picha Arusha aliyeshindwa kufuatilia kupata maelekezo
ya Mkurungezi wa Wanyamapori kuhusu mtumishi wake aliyekiuka Sheria
katika utoaji wa vibali. Aidha, alishindwa kupeleka kwa Katibu Mkuu
taarifa kuhusu mtumishi huyo ili achukuliwe hatua za nidhamu.
(i) Silvanus Atete Okudo – amepewa Onyo Kali la Maandishi.
(5) Wafuatao ni Maafisa ambao uchunguzi dhidi yao unaendelea:
(i) Bw. Mohamed Madehele – Ofisi ya Matumizi Endelevu ya Wanyamapori
(ii) Bibi Mariam Nyallu – Kituo cha Uwindaji wa Kitalii, CITES na Utalii wa Picha – Arusha.
Wahusika
wengine katika kadhia hiyo wasiokuwa waajiriwa wa Wizara ya Maliasili
na Utalii watachukiliwa hatua na mamlaka nyingine husika.
[MWISHO]
Mhe. Khamis Suedi Kagasheki
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII
13 Agosti 2012
No comments:
Post a Comment