13 July 2012

Breaking newz............OKWI APATA ULAJI BUNDESLIGA, ANAENDA JUMAPILI KUJARIBU BAHATI

Okwi


KLABU inayomtaka mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, FC Red Bull Salzburg ya Austria yenye maskani yake Wals-Siezenheim, ikitumia Uwanja wa Red Bull Arena,
ikiwa zaidi inafahamika kama SV Austria Salzburg kabla haijanunuliwa na kampuni ya Red Bull mwaka 2005, imewahi kufika Fainali ya Kombe la UEFA mwaka 1994 na inacheza Ligi Kuu ya Austria, iitwayo Bundesliga kama Ligi Kuu ya Ujerumani.
Timu hiyo ni kama timu ambayo Okwi, anachezea kwa sasa, Simba SC, kwani nayo inavaa jezi za rangi ya nyeupe na nyekundu na imewahi kutwaa taji la Bundesliga ya Austria mara saba na pia ilicheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 1994–1995 kama Casino Salzburg, na kuwa timu pekee, ambayo haikufungwa na mabingwa wa wakati huo, Ajax Amsterdam.
Okwi ambaye awali ilielezwa atakwenda Italia katika klabu ya Parma, sasaimegundulika anaenda kufanya majaribio FC Red Bull Salzburg na ataondoka Uganda Jumapili.
Okwi ameikosesha Simba Sh. Bilioni 2 kwa kukataa kujiunga na klabu ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini na kuamua kwenda Austria.
Okwi hivi Jumapili anaenda Austria kufanya majaribio katika klabu ambayo iko tayari kutoa Euro 600,000 akifuzu na si Italia kama ilivyoelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ wiki mbili zilizopita.
Uchunguzi wa kina uliofanywa  umegundua Okwi ataondoka mwishoni mwa wiki Uganda kwenda Austria na hadi mwishoni mwa wiki nyingine tayari itajulikana kama amefuzu au la.
Awali Olando Pirates ya Afrika Kusini ilimuomba Okwi akafanye majaribio huko kama angefuzu wangemsajili dau la dola 550,000 kabla ya kuibuka kwa taarifa za kutakiwa Italia na klabu ya Parma.
Hata hivyo, Simba SC ilisema imeshindwa kumshawishi Okwi kwenda kucheza Afrika Kusini kwa kuwa mwenyewe anataka kucheza Ulaya tu. Wakala aliyeiunganisha Simba na Pirates akawasilisha ofa nyingine kutoka Mamelodi, ambayo ni Euro 600,000 na kupanda hadi Sh. Bilioni 2, lakini bado mabingwa hao wa Tanzania, walishindwa kumshawishi Okwi kwenda Ligi Kuu ya Afika Kusini (PSL). 
Na Mahmoud Zubeiry

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname