SIMBA SC imetwaa ubingwa wa Kombe la Urafiki, baada ya
kuifunga Azam FC kwa penalti 3-1 usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,
kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
Penalti za Simba zilikwamishwa nyavuni na Mwinyi Kazomoto,
Amir Maftah na Kiggi Makassy, wakati Haruna Moshi Boban alipaisha na kwa upande
wa Azam FC, aliyefunga ni Hamisi Mcha ‘Vialli’ pekee, wakati Samir Hajji Nuhu
ilidakwa na Juma Kaseja, Ibrahim Mwaipopo ilipanguliwa na Himid Mao ‘iliota mbawa’.
Kabla ya matuta, mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix
Sunzu alitangulia kuifungia Simba dakika ya 29 kabla ya Hamisi Mcha ‘Vialli’ kusawazisha
dakika ya 45 na ushei.
Kipindi cha pili mchezo ulichangamka zaidi na dakika ya 81,
John Bocco ‘Adebayor’ aliyetokea benchi aliifungia Azam bao la pili, kabla ya
Kazimoto kuisawazishia Simba kwa penalti dakika ya 87, baada ya Danny Mrwanda
kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Kwa ushindi huo, Simba SC wamezawadiwa Sh. Milioni 10 na
Azam FC Milioni 5.
|
Wachezaji wa Simba wakimpongeza Sunzu (10) baada ya kufunga.
|
|
Aggre Morris wa kwanza kushoto, John Bocco wakimpongeza Viallli (wa pili kushoto) kufunga la kusawazisha |
|
Kikosi kilichoanza Azam |
|
Kikosi kilichoanza Simba |
HARUNA MOSHI NA UHURU SULEIMANI WAKIWA WAMEBEBA KOMBE
CHANZO-BIN ZUBERY BLOG
No comments:
Post a Comment