Matokeo hayo yametenguliwa katika kesi ya pingamizi la ushindi wa Mbunge huyo iliyofunguliwa na mgombea wa CHADEMA, Mwalimu Norbet Joseph Yamsebo kufuatia kasoro zilizojitokeza wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na madai ya kutoa rushwa kwa makundi mbalimbali ambapo watu wengi walijitokeza kutoa ushahidi na kukiri kuwa ni kweli walipokea vitu kama vile fedha, baiskeli, pikipiki, vinywaji, kinanda kwa Kanisa Katoliki n.k.
Kiti hicho kilichokuwa kikishikiliwa na Aeshi Khalfan Hilaly, CCM, sasa kipo wazi.
No comments:
Post a Comment