Kama upo kwenye position nzuri lakini hauwapi motisha wala kuwasapoti rafiki zako waweze kusogea kufikia mafanikio yao basi nawewe ni sehemu ya tatizo na sio suluhisho. Kuna watu huwa tunaamini kwamba rafiki yako anapofanikiwa anaweza kuja tengeneza nguzo nzuri na imara ya kuweza kuwasaidia nyie mlio nyuma yake ili mfikie alipo yeye, lakini kiuhalisia ni wachache sana wanaofanya hivyo kwakua wengi hupenda kuonekana wapo juu ya wenzao na ni bora kuliko wenzao.
Hata kwenye mitandao ya Kijamii kuna watu daily kuwapost na kuwasapoti watu wenye majina ambao hata hawafahamiki kwao, lakini wanashindwa kuwasapoti rafiki zao wenye biashara kupitia mitandao hiyo hiyo ya kijamii ili waweze kuinuka . Badala ya kuwanyooshea kidole na kuwadhihaki na idea zao au biashara zao ndogo, kwanin usiwashauri au kuwasapoti kwa pale padogo unapoweza? Ushauri pekeake unaweza kuwa na maana zaidi ya fedha utakayohic ukimpa iyamsapoti..
Kwanini usinunue pochi kwa best ako badala ya kwenda nunua posta ambayo ina ubora sawa na bei sawa na pochi anayouza mwenzako? Badala ya kutangazia Brands na Makampuni makubwa kwe page yako, kwanin usimtangazie na best ako biashara yake? Mwisho wa siku ukiwa na shida ni huyu best ako ndiye atakayekusaidia na sio yule wa Pochi Posta wala supastaa wala brand au kampuni kubwa ulizozitangaza kwakua wao hawakujui. Wengi tunaogopa kuwasaidia marafiki zetu kwakua tunajua wana vitu vya utofauti na tunajua ipo siku watatupita kimaisha, tunataka wawe katika levo ile ile ya maisha ili sisi tuwe juu yao na tujifanye kuwa kimbilio lao, tunasahau kwamba tukifanikiwa wengi na marafiki zetu inakua ni rahisi kutatua changamoto nyingi mbele yetu.
By Man Dea
#elimubiashara #mandeaideas
No comments:
Post a Comment