HATIMAYE mmiliki wa klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo (DRC), Moise Katumbi amekubali mshambuliaji wa kimataifa wa
Tanzania, Mbwana Samatta kujiunga na KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Mchezaji huyo alitarajia kurejea jana nchini kwa ajili ya safari ya Ubelgiji kwenda kuanza maisha mapya katika soka la Ulaya.
Samatta tayari amekwishasaini mkataba wa awali na Genk wa miaka minne na sasa anakwenda kukamilisha taratibu zilizobaki.
Samatta na Genk wanataka kukimbizana na muda ili kuwahi kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili.
Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo alisema kuwa hatimaye Katumbi
ameridhia Samatta aende klabu anayoipenda ili kuendeleza soka lake.
Katumbi alikuwa anataka Samatta aende Nantes ya Ufaransa, ili kucheza
soka huko, lakini mchezaji huyo hakupenda kwenda huko na alikuwa tayari
kubaki Congo kumalizia mkataba wake unaomalizika Aprili.
No comments:
Post a Comment