Mkurugenzi
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) akizungumza na
waandishi wa habari ambao hawapo katika picha leo jijini Dar es Salaam
kuhusu uchunguzi wa sakata la watuhumiwa wa wizi wa makontena 329.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Upelelezi
wa Makosa ya Jinai Bw.Diwani Athumani (CP) alipokuwa akitoa ufafanuzi
kuhusu uchunguzi wa watuhumiwa wa wizi wa makontena kwa Mamlaka ya
Bandari na Mamlaka ya Mapato Tanzania.
Na Nyakongo Manyama-Maelezo
Tarehe : 30/11/2015.
Kufuatia
agizo laWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa la kuwataka watuhumiwa wa wizi
wa makontena 329 katika bandari ya Dar es salaam kuchukuliwa hatua na
Jeshi la Polisi, tayari Jeshi hilo limewashikilia watuhumiwa kumi na
mbili wanaohusika na wizi huo. Akiongea na waandishi wa habari leo
Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CP)
Diwani Athumani amesema kuwa, uchunguzi unaofanywa na wataalamu
waliobobea katika makosa ya uhalifu wa kifedha umeweza kuwabaini watu
kumi na mbili ambao wamehusika na wizi huo.
“Kati
ya watuhumiwa hao kumi na mbili, watano wanashikiliwa na Jeshi la
Polisi na saba bado wapo katika upepelezi na upelelezi utakapokamilika
watafikishwa mahakamani,” alisema Kamanda Athumani.Wanaoshikiliwa
kutokana na tuhuma mbalimbali ni Kamishna wa Idara ya Forodha na Ushuru
TRA Bw. Tiagi Masamaki, Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru na Bi. Habib
Mponezia, Msimamizi Mkuu wa Kitengo cha Ushuru wa Forodha.
Watuhumiwa
wengine ni pamoja na Bi. Eliaichi Mrema, Msimamizi Kitengo cha
Mawasiliano ya Kompyuta Bw. Haroun Mpande na Mchambuzi Mwandamizi wa
Masuala ya Biashara Bw. Hamis Omary.Aidha Kamanda Athumani amewaomba
wananchi wenye taarifa za ubadhilifu wa mali za Umma kuendelea
kulisaidia Jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment