14 December 2015

MAWAZIRI WATATU WA RAIS MAGUFULI WAZUA UTATA ,MENGI YASEMWA,

Hatua ya Rais John Magufuli kuteua na kuwaapisha mawaziri watatu kabla ya kuapishwa kuwa wabunge, imeibua utata huku wanasheria wakihoji jinsi gani watafanya kazi za Kamati za Bunge kabla ya Februari wakati chombo hicho cha kutunga sheria kitakapoanza shughuli zake.Kwa mujibu wa ibara ya 66 (1) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano, Rais ana mamlaka ya kuteua wabunge wasiozidi kumi ambao anaamini wanaweza kumsaidia katika utekelezaji wa majukumu yake. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname