KUSUASUA, kwa Rais John Magufuli, kutangaza Baraza la Mawaziri
kunatokana na msimamo wake wa kuwachambua watu anaotarajia kuteua katika
nafasi hiyo huku akiaandaa mikataba ya makubaliano itakayokuwa mwongozo
kwa mawaziri hao. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).
Nia ya Rais, hadi kufikia hatua hiyo imetafsiriwa kwamba anataka kupata mawaziri ambao wataweza kwenda sambamba na kasi yake pamoja na wawajimbikaji.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kinaeleza kwamba kwa sasa Rais Magufuli, anasuasua kutangaza baraza lake
kutokana na kile kinachodaiwa ni kuandaa mikataba ambayo mawaziri baada
ya kuteuliwa watalazimika kuisoma kwa muda wa siku mbili kabla ya
kukubali uteuzi huo.
Chanzo hicho, kilieleza kwamba wale watakaokubali itabidi wasaini mkataba huo ili kukukabiliana na matakwa mkataba huo.
“Kwa sasa huyu jamaa anaandaa mikataba kwa ajili ya kuwapatia Mawaziri
na Manaibu wake na wanatakiwa kuisoma ndani ya siku mbili na yeyote
atakayekubaliana na mkataba huyo atalazimika kuisaini.
“Mikataba ya Mawaziri na Manaibu inalenga kuwabana watumishi hao na
kukubaliana kuwa iwapo itatokea tatizo katika wizara husika wao watakuwa
wa kwanza kuwajibishwa.
“Mkataba unalenga kuwafanya Mawaziri hao na Manaibu wao kuhakikisha
wanafanya kazi kwa uaminifu, uadilifu, na kwa kujali maslahi ya jamii,”
kilisema chanzo hicho.
Pia kilisema mkataba huo unaonekana unamasharti kwamba endapo siku
mawaziri hao watajiingiza kwenye vitendo vya kifisadi au Wizara husika
kulaumiwa watalazimika kujiuzulu bila kubembelezwa huku mhusika
akifishwa kwenye vyombo vya sheria bila mjadala.
Aidha, chanzo hicho kiliongeza kuwa kwa sasa wabunge waliowengi
wanaogopa nafasi za uwaziri na unaibu kwa madai kuwa kasi ya Rais
Magufuli ni kubwa na inaweza kumtia hatiani mtumishi wakati wowote.
“Wabunge hao wanapata homa kubwa kutokana na hatua ya Rais Magufuli na
Waziri Mkuu Majaliwa kuonesha ushujaa wa ajabu kwa kuwashambulia vigogo
ambao wameshindikana katika vitendo vya ukwepa wa ulipaji kodi au
kufanya ubadhilifu katika maeneo mbalimbali ikiwemo bandari.
“Kitendo kinachofanywa na Rais Magufuli ni sawa na kumvua nguo Kikwete
(Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) kwani kwa madudu ambayo yanaonekana
inaonesha wazi kuwa nchi haikuwa na kiongozi na kama ilikuwa na kiongozi
basi kiongozi huyo alikuwa na mkono wake.
“Sikiliza kijana haiwezekani nchi ikawa na wafanyabiashara wakubwa na
matajiri wakubwa wanaokwepa kodi huku kiongozi wa nchi kwa kujua ama
kutokujua anakaa nao meza moja kwa kuwapongeza kwa misaada kiduchu
wanayotoa katika jamii huku wafanya biashara hao wakiongeza wigo
waliyonacho na wasiyonacho jambo ambalo ni hatari,” kilisema.
Wakati huo huo kuna tetesi kuwa kutokana na kasi ya Rais Magufuli kwa
sasa ndani ya CCM kuna mvutano mkubwa ambapo wanataka kubadilisha katiba
ya chama hicho.
Mgongano uliopo kwa sasa ndani ya Chama ni kutaka kubadilisha katiba ya chama hicho ili rais asiwe mwenyekiti wa chama.
“Hofu hiyo inatokana na kasi ya Rais Magufuli na inasemekana akiwa
mwenyekiti watendaji wote ambao wapo maofisini kihasara hasara watakuwa
na wakati mgumu zaidi.
“Mbali na hilo kwa sasa inaonesha wale watu ambao walikuwa walikuwa
wanapatiwa madaraka kwa njia ya kulindana itakuwa hadithi kwani
waliowengi wanaweza kutimliwa,” kilisema chanzo hicho.
“Hata hivyo ndani ya CCM kuna makundi ambayo yanatamani Rais Magufuli
kutoa agizo la kuchunguzwa kwa mali alizonazo mtoto wa Rais Mstaafu wa
awamu ya Nne Ridhiwan Kikwete.
“Kila mtu anajua kwamba mtoto huyo ana mali nyingi na anamiliki zaidi
vituo vya mafuta na magari kibao sasa watu wanajiuliza mali hizo
amezipata wapi?
“Lakini hapa kuna jambo zito ambalo linaweza kuwa na manufaa kwa upande
wa upinzani kama kwa muda mfupi Rais Magufuli ameweza kufanya mambo
makubwa na kubaini madudu mengi inakuwaje kwa rais aliyepita kwa maana
nyingine hiyo inaweza kuwapa nguvu ya kumpeleka Kikwete (ICC),” kilisema
chanzo hicho.
No comments:
Post a Comment