Msemaji wa Bunge amesema kuwa hawajapata malalamiko rasmi kutoka kwa
wabunge kuwa wanahitaji kuongezea fedha hizo zifikie milioni 130
kutokana na kupanda kwa thamani ya dola ya Marekani.
Mbunge Ezekiel Maige amesema kuwa afadhali Serikali iwanunulie magari kabisa kuliko kuwapa fedha
Mbunge wa Temeke kwa tiketi ya chama cha wananchi CUF Abdallah Mtolea
amesema wapewe fedha wakanunue wenyewe, pia amedai kuwa bei ya gari Land
Cruiser(Mkonge) ambayo wabunge wanatakiwa kununua gharama yake sokoni
ni milioni 130
Awali baadhi ya wabunge walidai kuwa wapewe milioni 130 kutokana na kupanda kwa bei ya magari wanayotakiwa kununua.
No comments:
Post a Comment