Kitendo cha Rais wa Tanzania na Waziri Mkuu wake, Majaliwa Kassim Majaliwa kuigusa kiutaratibu na kisheria Mamlaka ya Bandari na Mamlaka ya Mapato kimetoa picha kwa wachambuzi kuhusu kile ambacho kilikuwa kinafanyika kuhusu rushwa/ufisadi unaoendelea katika Mamlaka hizo.
Kufilisika kiusanii kwa kampuni kama Home Shopping Centre wakati Uchaguzi Mkuu umebakiza wiki moja haikuwa ajabu kutokana na hali halisi ya utendaji wa mamlaka za nchi lakini kinachostaajabisha kwa sasa ni jinsi ambavyo mamlaka ya nchi imekuwa ikifahamu wakwepa kodi kuanzia wakuu wake mpaka waendesha gari la mizigo inayobeba makontena ambayo hajalipiwa ushuru.
Nimeshangazwa kusikia taasisi ya Rais Magufuli imedadavua mpaka kufahamu idadi ya makontena ambayo yameingia mitaani bila kulipiwa ushuru. Mshangao huu umenifanya kuangalia nyuma na kugundua kuna kampuni ambayo ilifilisika ghafla bila maelezo ya kutosha kisheria!
Tunafahamu there is no time limit for commencing proceedings for an indictable offence. Ninafahamu serikali inaendeshwa na principle inayosema, one is considered innocent unless proven guilty lakini hii haiwezi kutufanya tusipate mashaka kuhusu kufilisika kisanii kwa Home Shopping Centre na pia hakuwezi kuizuia serikali kupekuwa vitabu vyao hata kwa njia ya Piercing the corporate veil ili kuhakikisha kama walifanya biashara ndani ya taratibu na sheria za nchi.
Rais Mkapa aliwahi kusema, serikali ina mkono mrefu katika kazi zake. Natumaini serikali ya Rais Magufuli itawatendea haki watanzania wote katika msingi unaosema, you can run, but you can't hide.
Is Home Shopping Centre owner of one of 349 lost containers?
Majipu lazima yatumbuliwe!
By MsemajiUkweli/Jamii Forums
No comments:
Post a Comment