BARNABA BOY MSANII WA BONGO FLEVA |
IRENE PAUL MSANII WA BONGO MOVIE NA KAMAFA RADIO PRESENTER |
YOUNG DEE |
DOCTA D-ONE |
MO MUSIC MSANII WA BONGO FLEVA |
KABURU KIONGOZI WA SIMBA |
Mastar mbalimbali wa hapa nchini wamejitokeza kwa moyo wote
kushirikiana kwa karibu na shirika la
Global Peace Foundation Tanzania katika kuhamasisha Amani katika kipindi
hiki cha kuelekea katika uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika siku ya
tarehe 25 October 2015.
Global Peace
Foundation Tanzania ( GPFTZ) ni Tawi la Taasisi ya Kimataifa lisilo la
Kiserikali na isiyotengeneza faida Global
Peace Foundation (GPF) yenye makao makuu yake Washington DC, nchini Marekani na lenye matawi zaidi ya 16 duani, . Ni
shirika linalo hamasisha kutetea na kulinda Amani dunia , shirika hili linaamini ya kuwa “ Kwa Mungu sisi wote ni familia moja”
GPF inafanya kazi kwa karibu na mitandao ya kiserikali na
watu binafsi katika kuendeleza jamii, taifa na kujenga na kulinda misingi na maadili katika
jamii husika.
GPF ina rekodi nzuri ya kufanya kazi kwa karibu na kwa
mafanikio makubwa kuhamasisha na kulinda
Amani katika nchi mbalimbali dunia katika bara la Afrika, Asia, Ulaya na
Amerika.
Kwa upande wa Afrika, shirika hili limekuwa likijihusisha na
maswala mbalimbali ya kijamii katika nchi za Kenya, Uganda na Nigeria kudumisha
Amani kwenye ukanda wa Afrika.
Tarehe 31 August 2015 shilirika hili lilizindua Campaign yao
iliyojulikana kama “AMANI KWANZA” Kampeni hii imeandaliwa maalumu kwa malengo
yafuatayo:
§ Kuwahamasisha Wanawake na Vijana kuwa mabalozi wazuri wa kulinda na kuitetea Amani ya nchi yetu hasa
katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi
§ Kujiepusha na vitendo mbalimbali
ambavyo vinaweza kuchochea uharibifu wa Amani nchini
§ Kuhamasisha kila mmoja ashiriki uchaguzi kwa amani
Akizungumza na muandishi wetu, Ndugu Martha Nghambi, ambae
ni Mkurugenzi mkazi wa shirika hili alisema campaign inaendelea vizuri,
wamekuwa wakitumia social media zaidi kama vile kurasa za Faceboob, Twitter na
Instagram ili kuhakikisha wana wafikia vijana wengi zaidi ambao ni zaidi ya 60%
ya watanzania wote na pia ni kundi la muhimu sana katika kulinda amani. Hali kadhalika Martha alisema wametoa wimbo
maalumu wa kuhamasisha amani ambao umeimbwa na
mwana mziki maarufu Barnaba Boy
“ bofya hapa chini
kuuliza wimbo huo”
Kuungana na Global
Peace Foundation Tanzania kuhamasisha Amani nchini tafadhali wa follow:
Twitter: @globalpeacetz, Facebook: globalpeacefoundationtanzania na
Instagram globalpeacefoundationtanzania
No comments:
Post a Comment