Mgombea
Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Mohamed Shein akimnadi
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli mbele ya maelfu ya wananchi
waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi
Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.
Dkt
Shein emebainisha wazi kwenye mkutano huo wa kampeni kuwa Dkt Magufuli
ni mtu sahihi na anatosha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,amesema kuwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa awamu ya tano
atashirikiana nae kwa kila jambo kuhakikisha Tanzania inapiga hatua
zaidi kimaendeleo.
Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi
waliohudhuria mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Mnazi
Mmoja,kisiwani Unguja jioni ya leo.SOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment