Kiongozi Mkuu wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amejitokeza kumtetea
Dk. Wilbroad Slaa dhidi ya majibu yanayotolewa na baadhi ya watu
kufuatia hotuba yake aliyoitoa ikimtuhumu mgombea wa Chadema, Edward
Lowassa kuwa fisadi asiyefaa kuchaguliwa kuwa rais.
Zitto ametumia akaunti yake ya Facebook kutoa mtazamo wake na uamuzi
atakaochukua ingawa amekiri aliwahi kukwaruzana na Dk. Slaa alipokuwa
Chadema na kupelekea kuondolewa katika chama hicho.
Hivi ndivyo alivyoandika:
Slaa hayupo kwenye karatasi ya kura. Naona watu wanahangaika na
Slaa. Wengine tuliamua kukaa kimya kwani hekima inataka hivyo. Kwa kuwa
watu wameamua kumtukana Dkt. Slaa ni lazima tutoke kulinda haki yake ya
kusema yake. Tutatoka na tutaungana na Slaa kuwasema walio kwenye
Ballot. Slaa hayupo kwenye Ballot. Mwacheni. Jadilini hoja zake sio
kumjadili yeye. Eti hata watu wasio na rekodi yeyote ya kupambana na
ufisadi nchi hii leo wanainua midomo yao kumsema Slaa. Mmeanza.
Tutamsaidia Slaa, tutamaliza.
Sina mapenzi na Slaa. Alihusika kuniletea shida kubwa ya kisiasa
nilipokuwa napigania MISINGI. Hata hivyo naipenda zaidi Tanzania kuliko
tofauti zangu na Slaa. Ni lazima aheshimiwe na alindwe
No comments:
Post a Comment