15 September 2015

TUSKER FANYAKWELI KIWANJANI YAWAKUNA WAKAZI WA MBEZI BEACH NA KIMARA WIKI HII

Mpenzi wa bia ya Tusker na mkazi wa Kimara-Korogwe Deogratias Dominic akipokea zawadi yake ya mfuko na fulana toka Mtangazaji wa redio Efm na Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani katika hafla ya kuipongeza baa ya Miti Mitatu ya Kimara-Korogwe jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker.

Mteja wa muda mrefu wa bia ya Tusker na mkazi wa Goigi, Mbezi Beach aliyefahamika kwa jina moja tu la Chong akiifurahia bia hiyo huku akikabidhiwa zawadi yake ya fulana na Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Mbezi Beach Obedi Salema katika hafla ya kuipongeza baa ya Coast Pub iliyopo Tangi Bovu-Mbezi Beach jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Promosheni hii inaendelea mikoani pia huku lengo kuu likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa inayotuzunguka kufanya kweli linapokuja suala la utoaji huduma kwa wateja lakini pia kuzisaidia baa hizo kuongeza mauzo ya siku wakati wa promosheni.

Mteja wa bia ya Tusker na mkazi wa Tangi Bovu-Mbezi Beach Wilfred Mahamba akipokea zawadi yake ya fulana toka kwa Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Mbezi beach Obedi Salema katika hafla ya kuipongeza baa ya Coast Pub ya Tangi Bovu-Mbezi Beach jijini Dar es salaam mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker.

Mpenzi wa bia ya Tusker aliyefahamika kwa jina la Kikya Mathias akizungumza na mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habash kabla ya kupokea zawadi yake ya mfuko na fulana wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Coast Pub iliyopo Tangi Bovu-Mbezi Beach jijini Dar es salaam ambayo iliibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker. Akijiandaa kutoa zawadi hiyo (nyuma yake) ni Balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi. Lengo kuu la kampeni hii ikiwa ni kuzifikia baa mbalimbali jijini Dar na mikoani na kuzihamasisha kufanya kweli linapokuja suala la utoaji huduma kwa wateja lakini pia kuzisaidia baa hizo kuongeza mauzo ya siku wakati wa promosheni.

Steven Kiswanta ambaye ni mkazi wa Kimara, Dar es salaam akipokea zawadi yake ya fulana na mfuko toka kwa Msimamizi wa Mauzo ya Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ubungo Victor Mhindi wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Miti Mitatu ya Kimara-Korogwe jijini Dar es salaam ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilifunga kambi eneo hilo mwishoni mwa wiki kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na bia ya Tusker.


Mtangazaji wa redio Efm na Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani akikabidhi zawadi ya fulana na mfuko kwa mkazi wa Kimara-Korogwe Edson Nambie wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Miti-Mitatu iliyopo Kimara-Korogwe jijini Dar es salaam ambapo promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani ilifunga kambi katika eneo hilo siku ya Jumamosi kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wiki katika promosheni hiyo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname