Akihojiwa na redio station Mh.Lissu anasema ameshangaa sana maneno aliyoyasema jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari.
Anasema Dr.Slaa alikwisha kuteuliwa kuwa mgombea urais mwezi January na mwezi April akathibitishwa na kamati kuu,
Anaendelea kusema ameshangaa Dr.Slaa kusema Gwajima ndo alimleta Lowassa
jambo ambalo siyo kweli kabisa, yeye Dr. Slaa mwezi wa tano ndo alianza
kumtafuta Lowassa kwa kumtumia Gwajima
Anasema wakati Lowassa anapokelewa tarehe 27 July kwenye Kamati Kuu,
Dr.Slaa hakulala nyumbani aliporudi nyumbani mchumba wake alimtupia
mabegi nje na DR. alilala kwenye gari.
Anasema dr. slaa asiwadanganye watanzania tatizo ni urais na mchumba wake.
Anasema ameacha siasa tangu siku ya kikao cha kamati kuu alipoandika
barua ya kujiudhuru kwa nini amepokea mshahara wa mwezi huu?? kwanini
anaendelea kutumia gari la chama la katibu mkuu na nyumba aliyonunuliwa
na chama muulizeni awaambie kwanini anaendelea kunufaika na hayo yote
toka CHADEMA???

No comments:
Post a Comment