Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola ukiendelea pembezoni mwa Mkutano wa 70 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani. |
Sekretarieti
ya Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola wamesifu kazi iliyofanywa na
Tanzania kama Mwenyekiti wa Kikundi Kazi cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa
jumuiya hiyo ya kusimamia na kuimarisha misingi imara ya jumuiya katika
kipindi cha miaka miwili iliyopita.
Hayo
yamesemwa na Dkt. Josephine Ojiambo Makamu Katibu Mkuu wa Sekretarieti
hiyo, kwenye taarifa fupi ya utekelezaji wa kazi za Jumuiya kwenye
Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Madola uliofanyika Septemba 24, pembezoni mwa Mkutano wa 70 wa Baraza
Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.
Taarifa
hiyo ilieleza kuwa uongozi wa Mhe. Bernard Membe (Mb.), ambaye ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania umeibua
mbinu za kisasa za kutatua matatizo ya nchi wanachama zilizokuwa na
changamoto ya kuheshimu misingi na taratibu za Jumuiya ya Madola.
Waziri
Membe ambaye anamaliza muda wake wa uongozi kwenye kikundi kazi hicho
mwaka huu, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri
aliokuwa anaupata kutoka kwa Sekretarieti inayoongozwa na Kamalesh
Sharma, ambao ndio waratibu wa shuguli za Kikundi Kazi cha Mawaziri.
Vilevile ushirikiano aliopewa na Makamu Mwenyekiti wa Kikundi hicho Mhe.
Murray McCully, Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand pamoja na wajumbe
wengine wa Kikundi hicho maalum kimewezesha kazi za kuratibu kazi za
Jumuiya hiyo kuwa na mafanikio makubwa.
Masuala
mengine yaliyojadiliwa kwenye mkutano wa Mawaziri ni utekelezaji wa
maamuzi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo kuhusu uimarishwaji
wa mifumo ya tehama na nyenzo mbalimbali za kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi kwenye nchi wanachama uliofanyika mwaka 2013 Jijini
Colombo, nchini Sri Lanka.
Kwenye
mkutano huo pia Mhe. George William Vella, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Malta alitoa taarifa fupi kuhusu maandalizi ya Mkutano wa mwaka huu wa
wakuu wa nchi na serikali wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Novemba 2015,
nchini Malta.
No comments:
Post a Comment