MSANII wa muziki wa hip hop nchini
Marekani, Stephen Brown, amejikuta akiswekwa jela miezi minne baada ya
kupiga simu polisi akidai msanii mwenzake, Nick Minaj, ametaka kumuua.
Pombe zilimfanya Brown, mwenye miaka 24, apige simu kituo cha polisi na
kudai mwanadada Nick Minaj alitaka kumuua, lakini polisi walipofika eneo
la tukio wakamkuta akiwa peke yake amelewa.
Kutokana na kitendo hicho cha kuwasumbua polisi, Brown amehukumiwa kifungo cha jela kwa miezi minne.

No comments:
Post a Comment