The Choice

04 September 2015

PROFESOR LIPUMBA ASEMA -- Mimi na Dk Slaa Ndio Wapinzani



Dk Slaa na Lipumba
Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), profesa Ibrahim Lipumba amekanusha taarifa kuwa yeye na Dk. Wilbroad Slaa wana mpango wa kudhoofisha upinzani kutokana na uamuzi waliouchukua katika hatua za mwisho.
Taarifa hizo zilieleza kuwa pamoja na mambo mengine, wawili hao wameamua kuudhoofisha upinzani baada ya kunyimwa nafasi ya kugombea urais kupitia Ukawa na badala yake nafasi hiyo alipewa Edward Lowassa aliyetokea CCM.
Akiongea na Azam TV, Profesa Lipumba amesema kuwa wao ndio wapinzani hasa na kuonesha jinsi walivyoumia kutokana na uamuzi wa Ukawa kumkaribisha Edward Lowassa na kumpa nafasi ya kugombea urais huku wakiacha msingi wa hoja yao ya kupata katiba mpya.
“Wapinzani ni sisi, ukisema wapinzani ni sisi… mimi nimekuwa mwenyekiti wa Chama Cha CUF toka mwaka 1999. Niliingia katika mapambano wakati kura zimeibiwa Zanzibar, tumefanya maandamano nimevunjwa mkono, nikaibiwa saa yangu na nimewekwa ndani,” alisema.
“ Sisi ndio wapinzani, wakati matukio haya yote yanatokea mheshimiwa Edward Lowassa hakuwemo katika mapambano haya, kwahiyo hauwezi kusema sisi tunavunja nguvu upinzani wakati sisi ndio vinara wa upinzani,” aliongeza.
Profesa Lipumba alijiuzulu uenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) siku chache baada ya kushiriki katika kumpokea Edward Lowassa ndani ya Ukawa akidai kuwa nafsi yake inamsuta.
Posted by Unknown at 18:27
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Comments system

Disqus Shortname

Social Widget

  • Instagram
  • The Choice
  • Twitter

Facebook

Flickr Widget

Boxed Version (yes/no)

IMG Scroll Animation (yes/no)

Widget Recent Post No.

Widget Random Post No.

Widget Recent Comment No.

PageNavi Results No.

Social Media Icons

  • choice

Ola

  • Download New Music
  • New Video
  • Nunua Gari Hapa
  • Contacts
New Video

Bofya hii PICHA kudownload APPLICATION YA The Choice

Bofya hii PICHA kudownload APPLICATION YA The Choice

pin blw

google analytics

Random Posts

Most Recent

Social Media Icons 2

  • The Choice

Contact us

Name

Email *

Message *


Total Pageviews

.

.

.

.

Popular

  • KUHUSU MIMBA YA ZARI KUHARIBIKA
  • MAGUFULI AHUTUBIA KISIWANI PEMBA LEO,AAHIDI KUULINDA MUUNGANO KWA NGUVU ZOTE
  • Eggy wa Masogange amlaumu SINTAH kwa kuvujisha video yake ya utupu
  • DAU NONO LIMETOLEWA KWA WATAKAO WABAINISHA WALE WALIO MVUA MWANADADA NCHINI KENYA
  • TAZAMA SHABIKI HUYU WA KIKE AKIWA NA BIKINI ALIPOVAMIA UWANJANI WAKATI MECHI IKIENDELEA
  • K LYNE ATAMBULISHWA NA MENGI HUKO MERERANI.
  • BREAKING NEWS,KIKOSI CHA TAIFA STARS CHATAJWA..BAHANUZI NDANI
  • ANGALIA PICHA...PREZOO ALIVYOPOKELEWA KENYA
  • MASTAA WAKUBWA AMBAO UMRI UMEWATUPA NA HAWANA WATOTO!
  • antivirus song-song of MR. Two a.k.a sugu.wmv

Blog Archive

My Website List

Recent

Comments

Simple theme. Powered by Blogger.