Mwalimu Nelson Andrew akiwa na jeraha shingoni baada ya kujeruhiwa.
UKATILI! Mwalimu Nelson Andrew (23), amevamiwa na watu wanaodaiwa kuwa
ni vibaka na kumkata kwa kisu koromeo katika jaribio la kumtaka awape
fedha la sivyo wangemuua.
Akizungumza na Uwazi hivi karibuni, kaka
wa mwalimu huyo, Andes Enock alisema tukio hilo lilijiri saa nane mchana
wa Septemba 10, mwaka huu, wakati yeye na mjeruhiwa huyo wakipitisha
biashara ya vyombo hatua chache kutoka kwenye nyumba wanayoishi.
No comments:
Post a Comment