Hatimaye Diamond ameitaja tarehe
ambayo sura ya binti yake Tiffah itaoneshwa hadharani kwa mara ya
kwanza. Tarehe 20 Septemba ndiyo siku ambayo Diamond na Zari wamepanga
kuitambulisha sura ya mtoto wao Latiffah kwa ulimwengu, lakini kuna
jambo kubwa ambalo litaambatana na utambulisho huo.
Licha ya kuwa Tiffah mwenye umri wa mwezi mmoja ni balozi wa maduka ya
nguo ya Baby Shop, lakini video na picha za kwanza zitakazoonesha sura
yake kwa mara ya kwanza zimedhaminiwa na makampuni mengine pia ambayo
bado hajayataja.
Kupitia Instagram Diamond ameandika;
“Tareh 20|09|2015 kwa mara ya kwanza sura ya Binti yangu
@princess_tiffah tutaiweka hadharani…je ungependa kujua ni Kampuni gani
imedhamini Video na Picha yake ya kwanza????.. Mbali na kuwa balozi wa
#BABYSHOP ya @Msasanicitymall & @Pugumall ungependa kujua amekuwa
Balozi wa nini tena???.. uskae mbali na mimi… #TiffahsDay inakaribia..%)
#ProudDad
(On the 20th of September 2015 my Daughter’s face @princess_tiffah will
be Exclusively shown for the first time to the public… would you like to
know which companies have sponsored her first video and photo??? Apart
from being @MsasanicityMall and @PuguMall #BABYSHOP brand Ambassador
would you like to know which companies have endorsed her??? Stay with
me!!! #TIffahsDay Coming Soon..%)”
Toka hit maker huyo wa ‘Nana’, Diamond na mpenzi wake Zari wamlete
duniani mtoto wao Tiffah mwezi mmoja uliopita, wamekuwa wakipost picha
bila kumuonesha sura yake hali ambayo imeongeza shauku ya mashabiki
kutaka kumuona.

No comments:
Post a Comment