.
Septemba
29, 2015 Dar es Salaam, Kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani,
imeendelea tena kuchukua sura nyingine wiki hii kwa wakazi wa jiji la Dar
sambamba na mikoa ya Mwanza, Moshi, Mbeya, Arusha na Morogoro ambapo imeendelea
kuziibua baa mbalimbali katika miji yote hiyo kama baa za wiki kupitia promosheni
ya kila wiki inayodhaminiwa na bia ya Tusker kutoka Kampuni ya bia ya
Serengeti.
Kwa upande wa Dar es salaam, baa
zilizotangazwa kwa wiki hii ni pamoja na Friends Pub ya Segerea na Check Point
ya Chanika ambapo kama ilivyo ada siku ya Ijumaa Kampeni hii ilitikisa eneo la
Segerea-Mwisho ambapo ndipo inapopatikana baa hiyo na kisha kuelekea Chanika
katika baa ya Check Point siku ya jumamosi, hii ikiwa ni mara ya pili kwa baa
hiyo kutembelewa na promosheni hii kutokana na wingi wa wateja wa bia ya Tusker
jambo ambalo liliwavutia mameneja wa bia hiyo.
Kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani
inaendelea kujizolea sifa katika umahiri wake wa burudani, muziki,
washereheshaji na zawadi kem kem kwa wateja wake huku ikirushwa moja kwa moja kupitia redio E-fm kuanzia saa
mbili jioni hadi saa sita usiku. Akizungumza na Mshereshaji wa promosheni hiyo
baada ya kupewa nafasi, mkazi wa Kinyerezi Zack Ngaweleja shabiki aliyefika
eneo la tukio katika baa ya Friends-Segerea alisema …“Nimekua mtumiaji mzuri wa
bia hii ya Tusker kwa miaka takriban mitano sasa na kikubwa kinachonivutia ni
ladha yake. Awali nimekua nikisikia tu matangazo ya promosheni hii kupitia
redio Efm na nikaona ni vema wiki hii nimeweze kujimuika na wapenzi wengine wa
bia hii katika kuipongeza baa yetu hii ya karibu”.
Kampeni ya Tusker Fanya Kweli Kiwanjani
imemaliza takribani wiki saba sasa ikizunguka baa kwa baa jijini Dar pamoja na
mikoani na hadi sasa imezifikia baa zaidi ya 400 ambapo haya ni mafanikio makubwa
kwa upande wa bia hiyo kutokana na kuvuka
nusu ya matarajio ikiwa kampeni hiyo bado inaendelea.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii
katika baa ya Friends Segerea, Meneja Masoko wa bia ya Tusker Bi Nandi
Mwiyombella alitoa pongezi na shukrani kwa mashabiki kufurika wakati wa
promosheni hiyo kusherekea na bia waipendayo ya Tusker huku akisitiza kuwa
Kampeni bado inaendelea na lengo likiwa ni kuzifikia baa 1000.
“Tunaendelea kuguswa katika kuwaonesha
wateja wetu kwamba tunawathamini na kuwashukuru kwa kuwa pamoja nasi katika safari
hii na waendelee kusherekea na kuburudika na Tusker”. Aliongezea kwamba Chapa
ya Tusker imejitosheleza katika kuhakikisha kwamba kampeni inakuwa kubwa na yenye
ubora wa kipekee ndani na nje jiji la Dar es salaam.
Promosheni hii ilienda sambamba na ile
iliyofanyika jijini Mwanza katika baa ya Siwa na Shooters siku ya Ijumaa na
Jumamosi. Baa hizi zilifanikiwa kujinyakulia ushindi wa kufanyiwa promosheni
hiyo baada ya kuzipiku baa nyingine sita zilizokuwa zikishindanishwa kwa wiki
iliyopita.
Ili kufuatilia kwa ukaribu kampeni
hii, wakazi wa Dar wanaweza kusikiliza kipindi cha Ubaoni cha E-fm ambacho
kinaruka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa tisa mchana mpaka saa moja
usiku na kufuatilia promosheni za Fanyakweli Kiwanjani zikirushwa hewani moja
kwa moja ni siku za Ijumaa na Jumamosi kuanzia saa mbili usiku. Mikoani Mbeya
ni Bomba fm katika kipindi cha “Afri carnival” kinachoruka kuanzia saa moja
hadi mbili na nusu jioni, Arusha ni Radio-5 kwenye kipindi cha
“Drive time antenna show” kinacho anza saa kumi na nusu hadi kumi na moja
jioni, Morogoro ni Planet Fm kwenye kipindi cha “Planet base show” kinachoruka
saa kumi na moja hadi saa mbili usiku na Kilimanjaro ni Kili Fm katika kipindi
cha “kili drive show” kinacho anza saa kumi na moja hadi kumi na nusu
jioni kwa maelezo zaidi.
No comments:
Post a Comment