Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe.
Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema hakuna
tofauti kati ya mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John
Magufuli na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa aliyechukua fomu ya
kugombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kutokana na wote kutokuwa na ubavu wa kupambana na ufisadi.
Zitto
alisema hayo jana katika mkutano mkuu wa ACT- Wazalendo Jimbo la Kigoma
Mjini, uliokuwa maalum kwa ajili ya kupiga kura ya maoni ili kupata
mgombea wa ubunge wa chama hicho Jimbo la Kigoma Mjini.
No comments:
Post a Comment