Mbunifu na Mmiliki wa Maduka ya Amina Design Ambaye pia ni Mentor wa Taasisi ya Manjano Foundation Amina Plummer Akitoa Mada kwenye Semina ya Kuwawezesha Wanawake Kuwa Wajasiriamali kupitia Vipodoz Vya Luv Touch Manjano Iliyoandaliwa na Manjano Foundation Kwa Lengo la Kuwajengea Udhubutu Wanawake Kufanya biashara pia namna ya Kujiwekea Akiba na Kutumiza Malengo yao. Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa Miradi ambayo itamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd Mama Shekhar Nasser (Katikati) Akiwa na Mbunifu Amina Plummer (Kushoto ) Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male.
Mbunifu na Mmiliki wa maduka ya Amina Design Amina Plummer ni mmoja kati ya Mentors 15 watakao wapa muongozo washiriki 30 wa mradi wa Manjano Foundation. Amina aliwapa somo la kujifahamu kama wajasiriamali chipukizi kuwa wasilimbuke pale ambapo mafanikio yanapo anza kuja. Aliwaeleza kuhusu umuhimu wa kujiamini, kumuamini Mungu, kuwakarimu wateja, kuweka akiba Akiwa Sambamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male
Mbunifu Amina Plummer ni mmoja katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo inayoandaliwa na Taasisi ya Manjano Kupitia Bidhaa za Luv Touch Manjano.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd Mama Shekhar Nasser na Mbunifu Amina Plummer Pamoja Afisa Mtendaji Mkuu wa Women an Youth Empowerment Program Kutoka Uganda Dada Remmie Male. Katika Picha ya Pamooja na Washiriki wa Semina hiyo..
No comments:
Post a Comment