Wakati
mwingine si kitu rahisi kupima ushawishi lakini tutaangalia ni wazo
mawazo gani ya mtu, mifano gani ya mtu, kipaji gani cha mtu na ugunduzi
gani wa mtu uliobadilisha jambo katika nchi yetu. Hawa ndio mastaa 20 wa
burudani, michezo na urembo Tanzania wenye ushawishi mkubwa zaidi
1. Wema Sepetu
Well, well, well
kunaweza kukawa na mjadala mrefu sana hapa wa kwanini mrembo huyu
akamate nafasi ya kwanza wakati kila kukicha amekuwa akigonga vichwa vya
habari kwa scandals kibao. Hiyo ni kweli lakini ukiugeuza umaarufu huo
wa Wema na kuupeleka katika muktadha wa biashara na jinsi
anavyokubalika,hakuna anayemfikia Wema. Wema ni brand inayouzika
kirahisi. Kuandikwa mara kwa mara
kwenyemagazeti ya udaku ambapo mara nyingi si kwa kupenda yeye, kumemfanya Wema awe dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu. Habari za Wema hapa Bongo5 zimekuwa zikipata hits (kusomwa zaidi) kuliko habari yoyote ya staa yoyote yule unayemjua hapa Tanzania.
kwenyemagazeti ya udaku ambapo mara nyingi si kwa kupenda yeye, kumemfanya Wema awe dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu. Habari za Wema hapa Bongo5 zimekuwa zikipata hits (kusomwa zaidi) kuliko habari yoyote ya staa yoyote yule unayemjua hapa Tanzania.
Iwe picha akiwa kwa
daktari aking’olewa jino, picha za mtindo mpya wa nywele, tattoo
aliyojichora, picha za mbwa wake, Gucci na Vanny, picha zinamuonesha
akiwa na shoga zake Kajala na wengine, kila kitu kuhusu Wema kinavutia
attention ya watu. Story za Wema husomwa zaidi na kupata comments nyingi
kuliko za wengine wote.
Kama leo hii Wema
akisema aanzishe bidhaa yoyote inayowalenga vijana, haitachukua muda
kushika na kutafutwa kama njugu. Wema ni show stopper! Kama akiingia
ukumbini kwenye shughuli, shughuli hiyo husimama kwa muda kutokana na
watu kugeuka kutaka kumwangalia kwa uzuri zaidi wakati akielekea sehemu
ya kukaa. Kutoka kuwa Miss Tanzania na sasa akiwa muigizaji wa orodha A
Tanzania, CEO wa kampuni ya filamu, Endless Fame Films, Wema Sepetu ni
mwanamke mwenye ushawishi mkubwa.
2. Diamond
Ni msanii gani Tanzania
ambaye nyimbo zake zinahit mtaani bila hata kupigwa redioni? Bila shaka
umeshasikia nyimbo nyingi za Diamond mtaani siku za hivi karibuni
ukiwemo UKIMWONA na ukajiuliza iweje unahit wakati haujaachiwa rasmi?
Muziki wa Diamond umekuwa ukitumika kama tulizo la wanyonge walio kwenye
mahaba mazito. Kuanzia Mbagala, Nitarejea, Lala Salama, Mawazo ama
Nataka Kulewa, zote zimekuwa zikitumiwa na watu wa rika mbalimbali,
madaraja tofauti ya kiuchumi, wanawake kwa wanaume na watoto kama
burudisho la roho zao. Diamond Platnumz hi hitmaker na haoneshi dalili
za kupunguza kasi.
Diamond ndiye msanii
anayefanya show nyingi zaidi ndani na nje ya Tanzania na kwa kulipwa
gharama kubwa kuliko msanii mwingine yeyote muda huu. Hujaza kumbi kubwa
za starehe yeye mwenyewe bila backup ya msanii mwingine na kuwaacha
wasichana wakibubujikwa na machozi ya furaha na kutamani walau kukishika
tu kifua chake kilichoanza kupasuka kwa mazoezi.
Kwa mujibu wa kampuni ya
Push Mobile, Diamond ambaye jina lake halisi ni Nasib ndiye msanii
anayeuza zaidi nyimbo zake kama miito ya simu (RBT).
Pamoja na kuzungukwa na
scandal kibao kuhusu wanawake, Diamond ni kijana mwenye mawazo pevu na
ya kiutuuzima. Akiwa ametoka kwenye familia duni na kupata misukosuko
mingi ikiwemo kutengwa na baba yake na kulelewa zaidi na mama yake,
Diamond amekuwa akitoa ushauri na kuwapa moyo watafutaji wa maisha
wasikate tamaa. Hupenda kutoa ushauri kwa vijana wenzie kuhusiana na
umuhimu wa kujituma, kuchapa kazi, kumuabudu mwenyezi Mungu na kutokata
tamaa.
Katika kuhakikisha kuwa
anaitolea pia jamii, hivi karibuni alitangaza kuwa na nia ya kujenga
msikiti. Ni kwa sababu zipi kijana huyu asiwe na ushawishi?
3. Millard Ayo
Japo si kituo chake cha
kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia
kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na
ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya
burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP.
Kuondoka kwake Radio One
kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia
Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho
kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa.
Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora
kabisa Clouds FM.
Leo hii Millard ni
miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si
maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye
mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers
40,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 90,000.
Umaarufu wake kwenye
mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni
makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet.
Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake
binafsi yenye wasomaji lukuki. Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard
ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata
sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.
4. Nancy Sumari
Nancy Sumari ni msichana
mrembo, mpole na mcheshi. Ndiye Miss Tanzania wa kwanza aliyewahi
kufika mbali zaidi kwenye shindano la Miss World ambapo mwaka 2005
alifanikiwa kuwa Miss World Africa.
Kwa sasa Nancy ambaye ni
mama wa mtoto mmoja wa kike, ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam na anasoma Shahada ya Biashara. Pia ni mjasiriamali na anafanya
kazi zake na jamii zikiwemo kuwahamasisha watoto wa kike kujitambua na
kuthubutu, ili kutimiza ndoto zao.
Katika harakati zake za
kuhakikisha wasichana wa Tanzania wanatambua haki zao, anaendesha
programu iitwayo Mentorship, ambayo inazunguka kwenye shule mbalimbali
za serikali za wasichana nchini, na kuzungumza nao kuhusu maisha.
“Kwenye programu hiyo, tunabadilishana mawazo na wanafunzi na wao
wanazungumza changamoto wanazokutana nazo na kupeana mawazo jinsi ya
kufanya kwani nawaambia wakiamua kuthubutu wanaweza kufanikiwa, na
wanaonesha wanaweza,”Nancy aliliambia gazeti la Habari Leo hivi
karibuni.
Pamoja na hayo pia Nancy
anashirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), kwenye kampeni ya
kujenga mabweni ya wasichana kwenye shule za sekondari za serikali
nchini, ili kuhakikisha watoto wa kike wanapata elimu.
Hivi karibuni alizindua
kitabu chake kwaajili ya watoto ‘Nyota Yako’ kinachomlenga mtoto wa kike
kuona jinsi wanawake wengine walivyofanikiwa licha ya kupitia
changamoto mbalimbali.
“Ninaamini kitabu
kitasomwa na wengi ndio maana nikaamua ujumbe wangu niufikishe kwa njia
hii, watasoma watoto wetu hata wajukuu kitajenga kitu kwenye akili ya
mtoto na wakisoma shuhuda za hao waliofanikiwa nao watathubutu”
aliliambia Habari Leo. Tanzania itegemee mengi makubwa kutoka kwa mrembo
huyu.
5. Ambwene Yesaya aka AY
Safari ya AY mpaka kuja
kuwa nyota anayefahamika Afrika nzima na sehemu zingine duniani haikuwa
rahisi. Amepitia mengi. Aliwahi kusema kuwa kabla ya kufahamika Afrika
Mashariki, alikuwa akienda Kampala na Nairobi kufanya show za bure ili
tu kukuza jina lake, jitihada ambazo zilizaa matunda.
AY ni msanii smart, mbunifu, risk taker na anayeijua biashara ya muziki.
Ni msanii wa Tanzania
anayefanya video za ghali zaidi ambapo mpaka sasa video zake tatu, Speak
With Your Body aliowashirikisha wamarekani Lamyia Good na Romeo,
Partyzone na Money zilimgharimu zaidi ya dola 70,000 kwa pamoja
kuzikamilisha. Video zake zimekuwa zikichezwa kwenye vituo vikubwa vya
runinga duniani.
Mwaka jana alifanikiwa
kuandika historia kwa kushinda tuzo za Channel O katika kipengele cha
video bora ya mwaka ya Afrika Mashariki kwa wimbo wake I don’t Wanna Be
Alone aliowashirikisha Sauti Sol wa Kenya. Umaarufu na busara zake
ziliivutia kampuni ya simu ya Airtel mwaka jana na kumteua kuwa balozi
wake. Kwa sasa ni mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya burudani, Unity
Entertainment, anajihusisha na biashara za nguo, mwanzilishi wa kipindi
cha televisheni cha Mkasi na biashara zingine.
Akiwa na followers zaidi
ya 40,000 kwenye Twitter, mwaka huu AY amekuwa msanii wa kwanza wa
Tanzania kupata alama ya tick ya blue ya verification kwenye mtandao
huo. Ni watu watano tu nchini wana alama hiyo.
6. Hasheem Thabeet
Hasheem Thabeet ni
mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi ya mpira wa kikapu wa kulipwa
nchini Marekani, NBA. Akiwa na urefu wa 7 ft 3 Hasheem ndiye mchezaji
mrefu zaidi kwenye ligi hiyo. Anacheza timu ya Oklahoma City Thunder kwa
mshahara wa dola milioni 5.128 kwa mwaka.
Pamoja na kuwa Marekani
muda mwingi, Hasheem hasahau ya nyumbani na hupenda sana kuongelea
wasanii wa Bongo Flava kama alivyoandika.
“Mwaka 2000 mpaka mwaka
2005 Juma Nature alikuwemo katika kila nyimbo ambayo ilikuwa hit ndani
ya bongo. kubali au kataa. #fact.”
Akitumia Twitter,
Hasheem anajulikana kwa jinsi anavyopenda kuandika ujumbe wa matumaini.
Hizi ni tweets 5 zenye ujumbe utiao matumaini alizoandika hivi karibuni.
No matter what u go thru
in life there is no need of gettin angry with god and reflect
bitterness to people around u. #havefaith.
The wise ones speak b’se
they have something to say… fools speaks b’se they have to say
somethin. thik before u speak. #liveandlearn.
Everything can change in a blink of an eye… but dont worry; god never blinks. #believe #havefaith
Life aint about how hard u can hit… it’s about how hard u can get hit and still move forward.
Envy is a waste of time… accept what you already have, not what u need.
7. Flaviana Matata
Flavy ni mwanamitindo wa
kimataifa aliyehamishia makazi yake nchini Marekani. Amefanikiwa kwa
kiasi kikubwa katika fani hiyo kwa kushiriki kwenye fashion show kubwa
dunia, kufanya matangazo ya brand kubwa pamoja na kuhusishwa kwenye
majarida ya kimataifa.
Hivi karibuni Matata alishiriki katika kampeni za matangazo makubwa ya makampuni ya nguo ya DIESELna EDUN.
Kampeni ya DIESEL + EDUN
ilianzishwa mwaka jana mwezi wa kwanza ambapo muanzilishi wa kampuni ya
DIESEL – Renzo Rosso – na waanzalishi wa kampuni ya EDUN – Ali Hewson
na Bono walisafiri hadi nchi za Uganda na Mali na kukutana na wakulima
wa pamba barani Africa.
Waliingia makubaliano ya
kutengeneza nguo maalum zitakazotokana na pamba ya wakulima hawa wa
Afrika na hivyo kuwanufaisha moja kwa moja. Hivyo basi nguo hizi
zinatangazwa kama kampeni ili kunufaisha bara la Afrika.
Nguo hizo zitaanza
kupatikana mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika maduka mbalimbali nchini
Marekani na duniani. Pia nguo za DIESEL + EDUN zitauzwa kupitia mitandao
mbalimbali.
Flaviana ambaye aliwahi
kuwa Miss Universe Tanzania 2007 anabaki kuwa mwanamitindo pekee kutoka
bara la Africa katika kushiriki katika kampeni za nguo hizo.
Alianzisha taasisi ya
Flaviana Matata Foundation inayohusika kuwasaidia wasichana kupata karo
ya shule, sare na mahitaji mengine muhimu. Pia hutoa mafunzo na misaada
kwa wanawake ili waanzishe miradi mbalimbali ili kujiongezea kipato.
8. Loveness Diva
Diva Love Loveness ni
mtangazaji maarufu zaidi wa vipindi vya usiku. Ujasiri wake wa
kuzungumza masuala ya mapenzi bila kificho umemtengenezea maisha ya
pande mbili, kupendwa sana na kuchukukiwa sana. Ana mashabiki wengi.
Mara kadhaa kauli zake
zimewahi kuleta mijadala mizito nchini lakini bado kipindi chake cha Ala
za Roho cha Clouds FM kimeendelea kuwa kipindi chenye wasikilizaji
wengi zaidi ukilinganisha na vipindi vingine vya aina hiyo katika vituo
mbalimbali vya radio nchini.
Diva pia hujihusisha na shughuli za kusaidia wasiojiweza kupitia mradi wake wa Diva Giving for Charity.
9. Masanja Mkandamizaji
Huenda watu wengi
wanaweza wakawa hawafahamu kwamba Masanja ndiye staa wa Tanzania mwenye
likes nyingi Facebook, 104,670 na zaidi. Masanja ni miongoni mwa
wachekeshaji wa kizazi kipya wenye mashabiki wengi zaidi. Umaarufu wake
umetokana na kipindi cha Ze Komedi kilichoanzisha EATV na sasa kikiwa
TBC 1. Pamoja na kuwa mchekeshaji, Masanja ni muimbaji wa nyimbo za
injili, mchungaji mtarajiwa na mambo mengine. Huzitumia akaunti zake za
mitandao ya kijamii kuchekesha na kuwafurahisha zaidi followers wake na
ni miongini mwa mastaa wanaopata comments nyingi zaidi kila wawekapo
status.
10. Mwana FA
Hamis Corlone Mwinjuma
aka Mwana FA ni rapper anayeaminika kuwa miongoni mwa waandishi bora wa
mashairi ya Hip Hop kuwahi kutokea katika muziki wa kizazi kipya nchini
Tanzania.
Jina lake lilianza
kuvuma mwaka 1998 alipotoa ngoma yake ‘Ingekuwa Vipi?’ akiwa na Jay Mo
na pia ‘Mabinti’ ambayo ilitayarishwa na Bonny Luv.
Mwaka 2003, ngoma yake
‘Alikufa Kwa Ngoma’ – ilimpa tuzo kama wimbo bora wa Hip Hop wa mwaka
kwenye Kili Music Awards. Mwana FA aliendeleza utemi kwa kuachia hits
kibao kama Unanitega, ‘Hawajui’ feat. Lady Jaydee, Habari Ndio Hiyo
akiwa AY, Bado Nipo Nipo, Unajijua Unanisikia, Yalaiti na ngoma ya hivi
karibuni Ameen.
Mwaka huu anasubiriwa kwa hamu kuachia ngoma yake mpya iitwayo Kama Zamani aliyowashirikisha Njenje.
Pamoja na kufanya
muziki, Mwana FA aliamua kwenda nchini Uingereza kuongeza shule yake
ambako alisoma shahada ya Finance katika chuo kikuu cha Coventry.
Ana mipango pia ya
kuendelea na masomo ya PhD siku za usoni. Kwa sasa ameanzisha pia
kampuni ya kusimamia wasanii iitwayo Lifeline Music Inc ambayo tayari
ina msanii mmoja aitwaye Maua Sama.
11. Salama Jabir
Salama ni mhasisi wa
kipindi cha Planet Bongo cha EATV ambacho enzi anakifanya kilichangia
ubora wa video za muziki wa Bongo Flava nchini kutokana na kasumba yake
ya kuzikosoa bila woga. Baada ya kuondoka EATV na East Africa Radio,
Salama alienda kusoma nchini Uingereza na kurudi kukaa nje kwa muda na
mambo ya habari. Alikuja kurejea tena na kipindi cha Mkasi kinachorushwa
EATV na kukifanya kuwa kipindi bora kabisa cha mahojiano nchini. Salama
ni mcheshi, mtundu na anaufahamu mkubwa wa masuala ya burudani. Namna
ya uulizaji wake wa maswali hufanya vipindi vyake kuwa na mvuto zaidi.
12. Fid Q
Fareed Kubanda si rapper
anayeheshimika tu kama mwandishi mkali wa mashairi, bali pia
anatambulika kwa kujihusisha kwake na shughuli za kijamii.
January mwaka huu,
Taasisi ya Under The Same Sun inayojihusisha na kutetea haki ya watu
wenye ulemavu wa ngozi, albino nchini, ilimtunuku ‘cheti cha shukrani’
kwa mchango wake katika kampeni ya shirika hilo.
Alipata cheti hicho
baada ya mwaka jana kujumuika na taasisi hiyo katika ziara yao ya kanda
ya ziwa akiwa kama muelimishaji kwenye vita dhidi ya mauaji ya ALBINO.
“Kujituma kwenye
uchapaji kazi na utaratibu wa kuwa na nidhamu kazini ni moja kati ya
vitu vilivyowafurahisha,” aliiambia Bongo5.
Pia mwaka jana Fid alikuwa akiendesha darasa la hip hop la hiari jijini Dar es Salaam.
Akielezea madhumuni
yake, Fid alisema, “Kwa haraka haraka hip hop darasa maudhui yake ni
kuwafundisha vijana wawe na positive thinking na attitude kwa jamii,
yaani wawe na fikira zilizopo katika mstari ulio sahihi na hata kitabia,
kwahiyo tunawajenga hivyo kupitia muziki wa hiphop.”
13. Lady Jaydee
Mpaka sasa Lady Jaydee
ana albam tano na hivi mwezi ujao ataachia albam ya sita aliyoipa jina
NOTHING BUT THE TRUTH. Ndiye msanii wa kike Tanzania anayeheshimika na
mwenye mafanikio zaidi. Jaydee ni mjasiriamali ambaye hutumia pia kipato
anachokipata kwenye biashara zake kusaidia watu wanaohitaji msaada
hususan watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo maalum.
Mwaka huu Lady Jaydee
ambaye ana likes zaidi ya 47,000 Facebook na followers zaidi ya 22,000
Twitter, aliweka historia kwa kufanikisha safari ya kuupanda mlima
Kilimanjaro na kuwa msanii wa kwanza wa kike nchini kufanya hivyo.
13. Jacob Stephen
Jacob maarufu kama JB,
ni muigizaji ambaye wachambuzi wa filamu za Tanzania wanadai kuwa msanii
pekee wa kiume anayeweza kufikia mafanikio ya marehemu Steven Kanumba.
Ni muigizaji wa kiume anayependwa zaidi kwa sasa na filamu zake zimekuwa
kivutio kwa watu wengi wa kila rika. Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 14
kwenye sanaa ya uigizaji.
Kwa sasa anamiliki
kampuni ya filamu iitwayo Jerusalem ambayo imesaidia kuwaibua wasanii
wengine akiwemo Rose Ndauka, Elizabeth Kiyumba ’Nikita’ na
wengine.Pamoja na kuwa muigizaji pia JB ni mhubiri wa masuala ya dini.
15. Jokate Mwegelo
Jokate ni mtangazaji wa
TV (Channel 0), muigizaji wa filamu, mwanamuziki na mjasiriamali.
Umaarufu wake ulianza aliposhiriki shidano la Miss Tanzania mwaka 2006
na kukamata nafasi ya pili na kupata ubalozi wa Redd’s na gazeti la The
Citizen.
Jokate amewahi pia
kushinda tuzo za ZIFF kama muigizaji bora wa kike. Pamoja na hivyo
hujihusisha na muziki pia ambapo amewahi kushirikishwa na AY kwenye
wimbo Kings and Queens na hivi karibuni amesikika kwenye wimbo wa Lucci,
Water up.
Hivi karibuni
alijiingiza kwenye biashara ya ubunifu wa mitindo kwa kuanzisha kampuni
na brand ya Kidoti ambayo hubuni nguo pamoja na kutengeneza nywele za
aina mbambali zinazopatikana nchini.
16. Vanessa Mdee
Vanessa ni mtangazaji
mahiri wa MTV Base na Choice FM. Uwezo wake mkubwa wa kutangaza, maarifa
kuhusu burudani na mambo mengine vimemfanya awe miongoni mwa
watangazaji wa kike wakali zaidi barani Afrika na wenye mashabiki
lukuki.
Vanessa amefanikiwa pia
kwenye muziki ambapoi alimake headline sana aliposhirikishwa na Ommy
Dimpoz kwenye Me and You iliyotoka mwishoni mwa mwaka jana. Sauti tamu
kwenye chorus hiyo iliwashtua wengi kwakuwa alikuwa akijulikana kama
mtangazaji tu.
January mwaka huu
aliachia single yake ya kwanza Closer. Ngoma hiyo ilipokelewa vizuri na
mashabiki wa muziki na miongoni mwa nyimbo zilizopata downloads nyingi
zaidi mtandaoni. Na sasa ametajwa kuwania tuzo za Kili kama msanii bora
anayechipukia huku wimbo Me and You alioshirikishwa na Ommy ukitajwa pia
kwenye vipengele kibao. Ashafanikiwa kushare stage moja na wasanii wa
kimataifa wakiwemo Mi Casa Music wa Afrika Kusini.
17. Rita Paulsen
Maadam Rita anafahamika
zaidi Facebook kwa wafuasi wake zaidi ya 25,000 kama mwanamke mwenye
ushauri muhimu kuhusu maisha. Ni mwanzilishi wa shindano kubwa la kusaka
vipaji vya kuimba nchini, Bongo Star Search ambalo limefanikiwa kutoa
vipaji vingi na kwa kuwazawadia washindi vitita vya pesa. Ni mcheshi,
mrembo na ambaye siku zote hupenda kuwapa moyo hata wale ambao uwezo wao
ni mdogo.
18. Profesa Jay
Profesa Jay ni miongoni
mwa wasanii waliyoifanya Bongo Flava ipate mafanikio. Akiwa na albam nne
mpaka sasa, Machozi Jasho na Damu 2001, Mapinduzi Halisi 2003,
J.O.S.E.P.H 2006 na Aluta Continua 2007, Prof amewahi kushinda zaidi ya
tuzo 6 mbalimbali zikiwemo za Kili. Mpaka sasa hits zake zikiwemo Bongo
Dar es Salaam, Jina Langu, Zali la Mentali, Nikusaidije na zingine
zinaendelea kutoa burudani isiyo na kifani katika masikio ya mashabiki
wake.
19. Dj Fetty
Fetty aka Fetilicious ni
Dj pekee wa kike wa Tanzania aliyefanikiwa hadi mwaka jana kupata shavu
la kwenda kupiga muziki kwenye jumba la Big Brother Africa. Ni msichana
mrembo, anayejiamini na machachari hewani huku akiwa na fanbase ya
nguvu. Ana likes zaidi ya 57,000 kwenye Facebook na followers zaidi ya
25,000 kwenye Twitter. Pamoja na kuwa mtangazaji wa kipindi pendwa cha
XXL, Clouds FM, Fetty ni dj kwenye club ya Ambassodors Lounge jijini
Dar.
20. Mzee Majuto
Kwa wengi King Majuto ni
mchekeshaji bora zaidi nchini kuliko wachekeshaji wote. Ni comedian wa
kuzaliwa ambaye sura yake tu huwavunja mbavu watu. Filamu zake zinauzika
zaidi huku akiwa na mashabiki kibao katika nchi zingine za Afrika
zinazozungumza Kiswahili. Umaarufu wake umemfanya apate deals za kufanya
matangazo mbalimbali yakiwemo ya Airtel na Azam.
“Jina la King Majuto
limeweza kuwa maarufu zaidi kwake, kutokana na kazi yake ya uigizaji
katika filamu za vichekesho, mafanikio yake katika uigizaji yamefanya
waigizaji chipukizi kutamani kumshirikisha msanii huyo mkongwe na
wengine kujifunza kupitia kwake. Wapo wasanii chipukizi ambao wanatamani
kufika kiwango alichofikia King Majuto, akitamba katika fani kwa zaidi
ya miongo mitatu sasa bila kuchuja wala kutetereka
No comments:
Post a Comment