19 August 2015

KISUMA NA SAFARI RESORT BAA ZA WIKI KWENYE SHINDANO LA TUSKER FANYAKWELI KIWANJANI



Mshereheshaji wa promosheni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani Gadner G. Habash akielezea utaratibu wa utoaji zawadi kwa wapenzi wa bia ya Tusker waliofika katika baa ya Kisuma wakati wa kuipongeza baa hiyo iliyopo Tandika jijini Dar es salaam. Baa hiyo ilibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker lengo likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli pale wanapotoa huduma kwa wateja.

Dj wa E-fm anayetambulika kwa jina la Dj Skit, akiporomosha burudani ya muziki ndani ya baa ya Safari resort ya Kimara jijini Dar wakati wa hafla ya kuipongeza baa hiyo iliyoibuka mshindi wa wiki wa kampeni ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani. Lengo la kampenii likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli wanapotoa huduma kwa wateja.

Balozi wa bia ya Tusker, Veronica Mbilinyi akipanga vizuri zawadi za bia zilizopangwa kutolewa kwa wateja mbalimbali wakati wa hafla ya kuipongeza baa ya Kisuma iliyopo Mwembeyanga Tandika mara baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker lengo likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli.

Mkazi wa Temeke Bi. Sikudhani Idd akituma salamu kwa marafiki zake kupitia redio Efm iliyokuwa ikisikika moja kwa moja kwenye kiwanja cha Kisuma wakati wa kuipongeza baa hiyo ya Tandika jijini Dar es salaam baada ya baa hiyo kuibuka mshindi wa wiki kwenye kampeni ya Fanyakweli Kiwanjani inayoendeshwa na bia ya Tusker lengo lake likiwa ni kuhamasisha baa mbalimbali za mitaa tunayoishi kufanya kweli pindi wanapotoa huduma kwa wateja. (Kushoto) ni Mshereheshaji wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani Gadner Habbash na (kulia) ni balozi wa bia hiyo Bi. Veronica Mbilinyi.

Mkazi wa Kimara Bw. Msua Kitalama akipokea zawadi ya fulana, mfuko na bia za bure toka kwa balozi wa bia ya Tusker Veronica Mbilinyi (Kushoto) wakati wa promosheni ya Fanyakweli Kiwanjani iliyofanyika katika baa ya Safari resort iliyopo Kimara jijini Dar es salaam. Baa hiyo iliibuka mshindi wa wiki wa shindano hilo baada ya kupigiwa kura na wapenzi wa bia hiyo kupitia redio E-fm.
MBU 0634.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname