Hussein Bashe
KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mjumbe wa mkutano mkuu CCM taifa Hussein Bashe amewaambia wanachama wenzake kukaza buti kwani uchaguzi wa mwaka huu ni mgumu.
Bashe alisema hayo wakati akiongea na wanachama wenzake na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho wilayani Nzega.
Alisema wanaCCM wanatakiwa kutambua kuwa uchaguzi wa mwaka 1995,2000,2005,2010 na huu 2015 kuna tofauti kubwa hivyo wanatakiwa kujipanga.

No comments:
Post a Comment