Ni
kitu ambacho tumezoea kukiona kwenye club kubwakubwa za soka duniani
kama Real Madrid, Manchester United, Arsenal, Barcelona na nyinginezo….
ni njia nyingine ya ubunifu inayokuza sana uchumi wa club husika.
Club ya
soka ya Simba ya Tanzania nayo imetangaza mpango wao mpya July 31 2015
ambapo mkuu wa idara ya habari Simba Haji Manara amesema >>> ‘August
1 2015 tutazindua rasmi maduka yatakayouza jezi za Simba, mabegi,
vipeperushi, kalamu na vitu vingine, yameshaanza kuuza toka July 31
lakini ni lazima tuyazindue rasmi‘
Kwenye sentensi ya pili Manara amesema ‘moja
ya hayo maduka ya Simba litakua pale Mlimani City shopping mall Dar es
salaam ambalo litauza kama mnavyoona timu za Ulaya, Simba ni club kubwa
na lazima twende na wakati uliopo, hatuwezi kuishia kuvaa jezi tu
nadhani wenzetu huko mbele watatuiga ndio kawaida Simba huwa inaanza
wengine wanafatia’
July 31 2015 Simba imetimiza miaka 44 tangu Simba izindue jengo lake ambalo lilianza kujengwa mwaka 1969.
“Kuhusu
Mavugo kutokuja Tanzania nimeona kwenye gazeti nimesikitishwa sana,
wiki iliyokwisha gazeti hilohilo liliandika Okwi anarejea Msimbazi
hatochezea tena klabu yake ya Denmark wakaandika bila kuweka chanzo
walikozipata habari, pia bila kubalance story’
‘Yani
naumia sana, taaluma gani hiyo? simu zetu zote zipo wazi kwanini
msipige kuthibitisha? nawahakikishia Mavugo siku ya tarehe 8 August
atacheza mechi ya Simba day “>>> Haji Manara
No comments:
Post a Comment