Mgombea
Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi ndugu John Pombe Magufuri amerudisha
fomu ya kugombea urais wa Jamhuri katika ofisi za tume ya taifa ya
uchaguzi (NEC) muda huu.
Katika
tukio ambalo limekuwa na kivutio kikubwa kwa watumishi wa NEC,
waandishi wa habari na wananchi waliokuwa wakipata huduma katika jengo
la NEC ni kitendo cha mgombea huyo kuacha kutumia lift na kupanda
ghorofa saba za jengo hilo kwa miguu.
Katika kile kilichoonekana
kuwa ni kudhihirisha hali nzuri ya Afya yake, Magufuli amewataka
viongozi wa CCM alioongozana nao katika tukio hilo wapande na kushuka
kwa ngazi kama yeye.
Magufuli
pia alikubali ombi la waandishi la kupiga nae picha ya pamoja ya
Ukumbusho kabla hajatangazwa rasmi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.

No comments:
Post a Comment