18 August 2015

Bifu la Diamond na Alikiba limeisha? Meneja wa Diamond apiga picha ya pamoja na Alikiba


Kitu ambacho mashabiki wengi wa Music Tanzania na hata nje ya Nchi wangependa kusikia kinaweza kikawa kimekaribia,  Meneja wa Diamond, Salaam amepiga picha ya Pamoja na mpinzani mkubwa wa msanii wake, Alikiba.
Haijajulikana nini kinaendelea lakini inawezekana labda ugomvi wa wasanii hao wawili umefikia mwisho na labda tutegemee chochote kutoka kwa hao wasanii wawili. Kweli mbongo mpe picha story ataandika mwenyewe😂😂
Picha hiyo inaonekana imepigwa jana, ukiangalia vizuri kwenye hiyo picha utamwona Ne-yo kwa nyuma, Kwahiyo iko wazi kuwa meneja wa Diamond yupo Kenya pamoja na Alikiba. Kitu kingine cha kutegemea ni collabo ya Diamond na Ne-yo, Diamond alikutana na Ne-yo mwezi uliopita Afrika kusini na aliahidi kuwa kuna kitu kinafata kwahiyo inawezekana meneja wa Diamond yupo Nairobi kwa ajili ya kukamilisha collabo hiyo.
Alikiba ameenda jijini humo kwa ajili ya  Coke Studio ambapo pia ataungana na wasanii wengine wa Afrika kushirikiana na Msanii wa Marekani.924676_873149446100081_1465182151_n

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname