Shinikizo dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, la kumtaka akihame Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kuongezeka na katika timu yake ya ndani ni watu wawili tu wanaonekana kumtaka abakie ndani ya chama hicho. Habari za ndani ya vikao vya kujadili hatua za kuchukuliwa na Lowassa baada ya jina lake kukatwa kwenye mchakato wa kugombea urais kupitia CCM, zinasema kuwa wandani wake wanaamini kuwa hana atakachopata kama ataendelea kubaki kwenye chama hicho tawala.
"Kaka sikiliza, inavyoelekea shinikizo dhidi ya Lowassa ni kubwa sana. Watu wake wa ndani wanataka aondoke CCM. Wanaona kama amedhalilishwa mno,"kilisema chanzo chetu ndani ya vikao hivyo.
No comments:
Post a Comment