11 July 2015

PROF MARK MWANDOSYA ATOA YA MOYONI BAADA YA KUKOSA KUINGIA 5 BORA

Katika nyakati mbalimbali mataifa, na binadamu pia hupita katika vipindi vya majaribu (testing times). Majaribu hayo ni njia moja ambayo naamini Mwenyezi Mungu, muweza wa yote, humuimarisha mtu na huimarisha Taifa iwapo tunaweza kuyamudu. Hiki ndio kipindi tunachopita sasa kama Taifa. Kwa maneno hayo napenda, kwa unyenyekevu mkubwa, kuwashukuru, na kwa dhati kabisa, wale wote mliotuunga mkono kabla na baada ya kutangaza nia, wakati wa na baada ya kuchukua fomu za kuomba nafasi hiyo, kwa imani kwamba tunakidhi, na pengine tunazidi vigezo vilivyoorodheshwa.  

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname