Ripota wa Teamtz.com alimuuliza Ney, kuna ishu imetapakaa kitaani kwamba umechuku vyombo vyako kutoka kwa Mr T. Touch,wewe unaseamaje? Ney alijibu, “sio kweli”.
Kwa hiyo tutegemee ngoma kama kawaida ikiwa ni mkono wa Mr. T. Touch..
Teamtz.com ikamcheck Mr. T. Touch, muda huo wa saa 2 kasoro usiku Jumanne 21 Julai 2015, akaulizwa vipi Ney kachukua vyombo vyake vya muziki? Nae alijibu “sio kweli? Muda alikuwa Mabibo Jeshini, teamtz.com ikataka imfuate imrekodi ili kukanusha uvumi huo, Mr T. Touch alisema anakuja sio muda mrefu, kwa hiyo tukutane Sinza.
Baada ya nusu teamtz.com ikampigia Mr. T Touch ili aseme amefika wapi, simu yake iliita bila majibu hata baada ya kubwa kwa mara zaidi ya 3.
Kwa hiyo kama umesikia huu uvumi, ujue sio kweli? Lakini kwanini hili liibuke? Kuna kitu kisicho cha kawaida kilionekana kwa mtu wa karibu. Kama kuna kitu, tutajua, lisemwalo lipo kama halipo laja?
No comments:
Post a Comment