![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhhCZGZ8fLNaVORh2Fx4glHUgcOpUl2rfLIkeoICfqgafTH3fMbRBTPvAKSIrfe-w8jHNz0-WNQ7ineBqEV-mopdtkejMt2yx8K5K4DqUfmw4S9uVMPQH_XU6tl9hHM5hDdJUthV3qX-D8A/s400/img_5258.jpg)
Amesema iwapo itatungwa kanuni hiyo itawalazimisha baadhi ya wabunge
wenye tabia ya kususia vikao vya Bunge katika mazingira yasiyokubalika.
Kauli ya Prof .Mwandosya ilionesha moja kwa moja kuwalenga wabunge
wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao wamesusia vikao vya
Bunge mwanzoni mwa wiki hii japo hakuwataja.
Kwa pamoja wabunge hao wakiongozwa na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya
Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, walichukua uamuzi huo baada ya
kutoridhishwa na hatua ya Serikali ya kuwasilisha na kupitisha miswada
ya sheria ya mwaka huu inayohusu masuala ya gesi, mafuta na petroli.
Amesema kitendo cha kuodoka bungeni wakati rais wa nchi anatarajia
kulihutubia Bunge ni tukio la fedheha na halitakiwi kuungwa mkono.
Amesema duniani kote ujio wa rais katika Bunge ni jambo muhimu kitaifa.
Alieleza kwamba bora itungwe kanuni ya kuwalazimisha wabunge wote kuwapo
bungeni siku rais anapokwenda bungeni vinginevyo mbunge awe na sababu
maalum.
No comments:
Post a Comment