16 July 2015

LOWASSA! HIVI NDIVYO ALIVYOCHEZEWA RAFU NA CCM DODOMA!

Mzee Kingunge kaongea na vyombo vya habari, ameanza kwa kupinga mfumo uliotumika kuwachuja wagombea wa urais kupitia CCM.
Kingunge amesema "Kamati ya Maadili huko nyuma ilikuwa ni chombo cha kuandaa taarifa ili kuisadia Kamati Kuu katika kuwajadili wagombea" 
Amesema Kamati ya Maadili ya safari hii imefanya kazi isiyowahusu kikatiba kukata majina ya wagombe.
Kingunge amesema Kamati ya Maadili ya CCM yenyewe imekosa maadili ya kuheshimu katiba na taratibu za chama.
Amesisitiza Kamati ya Maadili haikuwa na madaraka ya kupeleka majina 5 kwenye kamati kuu, ambayo ilipaswa kuhoji wagombea wote 38. 

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname