|
Msanii maarufu wa
Muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama “Linah” (wa kwanza kulia)
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Video yake mpya
ijulikanayo kama” No Stress” inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni chini ya
udhamini wa Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut,
katikati ni Meneja chapa pombe kali toka SBL, Shomari Shija na Meneja uvumbuzi
SBL, Attu Mynah. Tukio hilo limefanyika makao makuu ya kampuni hiyo Chang’ombe
jijini Dar es Salaam. |
|
Msanii
maarufu wa muziki wa kizazi kipya, Estelina Sanga maarufu kama “Linah” (kulia)
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari hawapo pichani juu ya ujio wa video
yake mpya itakayokwenda kwa jina la “No Strees” ambayo inatarajiwa kuzinduliwa
hivi karibuni kwa udhamini wa Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake
cha Jebel Coconut ambapo yeye ni balozi wa Kinywaji hicho. (Wa pili) ni Meneja
chapa wa pombe kali SBL, Shomari Shija, Mkutano huo ulifanyika makao makuu ya
Kampuni hiyo, Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
|
Meneja chapa wa
pombe kali SBL, Shomari Shija (katikati) akiongea na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya udhamini wa uzinduzi wa video mpya ya msanii Estelina
Sanga “Linah” itakayokwenda kwa jina la “No Stress” kupitia kinywaji chake cha
Jebel Coconut. Kushoto ni Meneja uvumbuzi SBL, Attu Mynah, na kulia ni msanii
Linah. Tukio hilo lilifanyika makao makuu ya SBL Chang’ombe jijini Dar es
Salaam |
|
Meneja chapa pombe kali toka
SBL, Shomari Shija (kushoto) akiongea na waandishi wa habari hawapo Pichani juu
ya udhamini wa uzinduzi wa video mpya ya msanii maarufu Estelina Sanga a.k.a”
Linah”(katikati) wimbo ukijulikana kama “No Stress”. Wimbo huo umedhaminiwa na
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Jebel Coconut ambapo
msanii huyo ni balozi. (wa kwanza kulia) ni Doreen Noni Meneja wa msanii huyo
toka Kampuni ya Panamusiq inayosimamia kazi za Linah. Tukio hilo lilifanyika
makao makuu ya SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
|
Meneja uvumbuzi
SBL, Attu Mynah, (kushoto) akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani
kuhusu udhamini wa video mpya ya msanii “Linah” kupitia chapa ya Jebel coconut
toka SBL chapa ambayo msanii huyo ni balozi. Video hiyo inatarajiwa kuzinduliwa
hivi karibuni na itakwenda kwa jina la “No Stress” (Wa pili) ni msanii Linah na
wa kwanza kulia ni Meneja wa msanii huyo Doreen Noni toka kampuni ya Panamusiq
inayosimamia kazi za msanii huyo. (Wa pili) kushoto ni Meneja chapa pombe kali
toka SBL, Shomari Shija. |
|
Meneja chapa pombe
kali toka SBL, Shomari Shija (kushoto) akiongea na waandishi wa habari hawapo
pichani juu ya udhamini wa uzinduzi wa video mpya ya msanii maarufu Estelina
Sanga a.k.a Linah” (katikati) itakayojulikana kwa jina la “No Stress”.
Udhamnini wa msanii huyo unafuatia ahadi ya Kampuni ya bia ya Serengeti
kusapoti kazi zake baada ya msanii huyo kupata mkataba wa ubalozi wa kinywaji
cha Jebel Coconut toka SBL. (Kushoto) ni Meneja wa msanii huyo Doreen Noni toka
Kampuni ya Panamusiq inayosimamia kazi za msanii huyo. Tukio hilo lilifanyika
makao makuu ya SBL Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia
kinywaji chake cha Jebel Coconut imetangaza rasmi siku ya leo dhamira yake ya
kudhamini uzinduzi wa video mpya ya msanii Estelinah Sanga maarufu kwa jina la
kisanii “Linah” itakayo kwenda kwa jina la “No Stress”.
Video ya wimbo huo imefanyika nchini
Kenya na Afrika ya kusini ambapo kwa kushirikiana na menejimenti ya msanii
huyo, SBL imeweza kudhamini utengenezaji wa video hiyo ambayo hadi sasa
imeshakamilika huku Kampuni hiyo ikisubiria kuizindua rasmi kwa wananchi.
Hatua ya SBL kudhamini video ya wimbo
huo ni njia mojawapo ya Kampuni hiyo kutambua sanaa ya muziki hapa nchini
ambapo pia hapo awali Kampuni hiyo iliahidi kumsapoti msanii huyo mara baada ya
kupata mkataba wa mwaka mmoja wa kuwa balozi wa kinywaji cha Kampuni hiyo cha
Jebel coconut.
Akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa utoaji wa taarifa hiyo kwa umma, Meneja Uvumbuzi wa kampuni hiyo Attu Mynah alisema “Kampuni ya bia
ya Serengeti inatambua umuhimu wa Sanaa ya muziki hapa nchini na siku zote
inalenga kumuwezesha msanii aweze kufikia malengo ya ndoto zake. Tumeamua
kudhamini utengenezaji na uzinduzi wa video ya wimbo wa msanii Linah kwa kuwa
tunatambua uwezo wake na tungependa afike mbali zaidi kimuziki”.
,
alisema “Tunafuraha kwa kuwa Kinywaji chetu cha Jebel coconut kinaendelea
kujizolea mashabiki wengi kupitia ubalozi wake ambapo ameendelea kuitangaza
chapa hii sehemu mbalimbali za Tanzania. Kama SBL tunajivunia kudhamini baadhi
ya kazi zake na ni matumaini yetu kuwa kupitia udhamini huu ataendelea kufanya
vizuri zaidi katika ngazi za kimataifa”.
Jebel coconut
ni aina ya pombe kali yenye ujazo wa 250ml inayotengenezwa nchini Tanzania na
Kampuni ya bia ya Serengeti ambayo imebuniwa na kutengenezwa kwa ladha ya nazi
ambazo zinapatikana kwa wingi hapa nchini. Jebel pia ni kati ya pombe kali
zaidi ya 10 za kimataifa zinazosambazwa na kampuni ya bia ya Serengeti huku
walengwa wa kinywaji hiki wakiwa ni watu wazima na wenye umri wa kati.
**MWISHO**
No comments:
Post a Comment