31 July 2015

KAMPENI YA TUSKER FANYAKWELI KIWANJANI SASA KUTIMUA VUMBI MIKOANI

Kampeni maarufu ya Tusker Fanyakweli Kiwanjani inatarajia kutimua vumbi wiki hii kwa wakazi wa jiji la Dar huku ikitanua wigo wake mikoani baada ya kufanya vizuri kwenye kipindi chake cha kwanza.

Kampeni hii inayoletwa kwenu na Kampuni ya bia ya Serengeti imejipanga kusaidia baa mbalimbali za mitaa tunayoishi na kuzipigia promo ya huduma zake kwa wapenzi mbalimbali wa kinywaji cha Tusker.

Akizungumza kuhusiana na mchakato mzima  wa Kampeni hiyo Meneja chapa bia ya Tusker Bi. Sialouise Shayo alisema SBL kupitia chapa yake ya Tusker imejipanga kutembelea baa zaidi ya 1000 kwenye miji yote mikuu nchini ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Morogoro, Moshi, Mbeya na Mwanza.

“Uamuzi wa kuongeza muda wa promosheni hii ya Fanyakweli Kiwanjani ni kutokana na maombi mbalimbali hasa toka baa za mikoani kufanyiwa promo/shindano kama hili kwenye baa zao”…alisema Sialouise.



Akifafanua zaidi kuhusu ratiba ya promosheni hiyo kwa wakazi wa Dar na mikoani, Sialouise alisema taarifa rasmi ya maandalizi ya promosheni hii itatangazwa kwenye vyombo vya habari vya mikoa husika ili kuwajulisha wapenzi wote wa kinywaji cha Tusker kuhusiana na nini kinaendelea.

Aliongeza kuwa utaratibu wa kuchagua na kuorodhesha baa mbalimbali ili zipite kwenye kampeni hii haujabadilika ambapo wapenzi wa Kinywaji cha Tusker wanatakiwa kuzipigia kura baa wazipendazo ambapo anachotakiwa mtu kufanya ni kutembelea baa ya mtaani kwake na kunywa bia ya Tusker, kupiga picha na kisha kuweka picha hizo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii (Facebook na Twitter) za Tusker au kusikiliza redio E-fm kwa wakazi wa Dar es salaam na wa mikoani wasikilize redio zifuatazo kwa maelezo zaidi. Redio 5 (Arusha), Kili fm (Kilimanjaro), Metro fm (Mwanza), Planet fm (Morogoro) na Bomba fm (Mbeya)

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname