Hii ni story nyingine
kutoka kwenye ile ishu ya kuvamiwa kwa kituo cha polisi cha stakishari Jijini
Dar es salaam ambapo askari wane na wananchi waliuawa na wale waliotambulika
kama majambazi na kupora silaha kadhaa na kutoweka nazo.
Leo kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam
alijitokeza mbele ya wanahabari na kuja na mafanikio ya msako mkali
unaoendeshwa na jeshi la polisi ambapo hadi sasa majambazio watano wamekamatwa
huku watatu kati yao wakiwa wameuawa na jeshi la polisi,huku silaha zilizoibiwa
kukutwa katika maeneo ya mkuranga zikiwa zimefukiwa chini tayari kwa ualifu.
Sasa pamoja na mafanikio hayo polisi wanasema kuwa
bado kuna majambazi waliohusika na lile tukio hawajakamatwa na kuna silaha
nyingine bado hazijakamatwa,bahati nzuri jeshi la polisi limefanikiwa kukamata
majina na picha za hao ambao bado hawajakamatwa.
Majina yako hapa kama picha juu zinavyoonyeshwa na
kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam
MAJINA YA MOST WANTED
1-ABDULAZIZI AHMAD ABDULRASHID maarufu kama USTADH
ABDULAZIZI anaishi jijini Dar es salaam na ndiye kiongozi wa kundi hilo la
wahalifu.
2-SHABAN MOHAMED MTUMBUKA maarufu kama AMIR SHABAN
NDOBE
3-HANNAFI JUMANNE KAPELA
4-HASSAN HAROUNA ISSA maarufu kama DR SHUJAA
5-ZAHAQ RASHID NGAI maarufu kama MTU MZIMA
6-ABUBAKAR NGINDO maarufu kama ABU MUHAMMAD
7-KHAMIS RAMADHAN
Jeshi la polisi linaomba popote uonapo hizi sura
wajulishe polisi popote ulipo.
No comments:
Post a Comment