Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa
ya Uganda, Uganda Cranes, Emmanuel Okwi amesajiliwa na klabu ya Denmark
inayocheza kwenye Danish Superliga, SønderjyskE.
Okwi amesaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo kwa miaka mitano baada ya
kumaliza vipimo vya kiafya. Mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo, Hans
Jørgen Haysen alisema wamekuwa wakimfuatilia Okwi na wamefurahi
kumsainisha.
Kupitia website ya klabu hiyo, Jørgen alisema wamekubaliana na klabu
yake ya zamani, Simba kuhusiana na gharama za uhamisho. Okwi amejiunga
na timu hiyo ikiwa ni wiki chache tu baada ya kufunga ndoa.
No comments:
Post a Comment