Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
SINTOFAHAMU!
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoundwa na vyama vinne vya
Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD sasa upo njia panda kuhusu ujio wa
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa anayesemwa kutaka kutimka kutoka
Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Habari
kutoka ndani ya vyama hivyo zinasema, tangu kukatwa kwa Lowassa katika
kuwania kwake kuteuliwa kuwa mgombea urais, kumekuwa na shinikizo kubwa
kutoka kwa watu mbalimbali, wanaotaka kada huyo wa chama tawala
anayetajwa kuwa na wafuasi wengi ajiunge na Chadema, ili awanie nafasi
hiyo kwa tiketi ya Ukawa.
No comments:
Post a Comment