~~Usiku wa jana kuamkia leo July 19 2015 Diamond Platnumz kanyanyua
ushindi mwingine kwenye Tuzo za MTVMAMA2015, zilizokuwa zikitolewa
Durban Africa Kusini.
Leo Diamond alipost Video inayomwonesha staa wa Mitindo Bongo, mrembo
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akicheza wimbo wa ‘Mdogomdogo‘ alafu akaandikia
hivi >>>> ‘Mbona Bado, Mtanyooka tu..‘ >>>> @
diamondplatnumz
Baadae Jokate nae akaandika kwenye ukurasa wake wa @Instagram kuhusu video hiyo ambayo alimpost Diamond:
Tuki-support mtu ndio kama hivi matokeo yake mtu anatumia baadae
kukudhalilisha. Hii video aliyo-post kwanza ni TBT kama sijakosea mwaka
jana mwishoni nilikuwa sehemu na my friends
@bikira_wa_kisukumaakani-record na kumtumia@diamondplatnumz bila mimi
kujua. Kiukweli sijui kwanini walifanya hivyo. Nikaja kujua baadae sana
na nikaona sio big deal cause kila mtu anapenda mziki na sio dhambi
kucheza mziki wowote uupendao.
Ila kitendo cha@diamondplatnumz kwenda kuitafuta huko ilikokuwa hii video clip na kui-post leo najiuliza maswali mengi
1, anataka ionekana kama nilikuwa nashangilia ushindi wake?
Which is not bad hakuna ubaya hapo kama unaamini ushindi wake ni sifa
kwa taifa ila
2, Kwanini a-post na caption ya Na Bado Mtanyooka? Ili amkomoe
nani? Au kwasababu niko karibu saaana na @alikibaofficialanatafuta
kutuchonganisha? Ili iweje? Mimi I believe life goes on na kila mtu ana
uhuru wa kumpenda au kuwa karibu na yule apendaye na kum-support ndio
maana hata mimi nimekuacha na your new life
3, Pengine ni kweli anaendeleza zile hulka zake za
kudhalilisha wanaweke aliokuwa nao waonekane sio kitu just because
hawako na diamond platnumz chibu dangote. Which to me is just dead
wrong.
@diamondplatnumz hizi sio tabia tunazozitegemea kwa mtu anayejisema
anakomboa mziki wa Tanzania sio kwa kuweka visasi na fitna zako wazi
wazi hivi. Unatu fanya tukose imani nawewe zaidi na tunaogopa ku-support
cause hukawi kutugeuka.
Kuwa tofauti basi, onyesha mfano kwamba kweli hupendi beef unapenda
mziki wa Tanzania uendelee ila kwa ulichoki-post unaonyesha wazi UNA
visirani na hutaki mema unatafuta drama, kiki, vurugu unataka kila siku
uwe wewe tu ambazo kiukweli mimi binafsi siziwezi utaendelea kushinda
wewe tu katika hilo na sitashindana nawewe katika hilo kwasababu siwezi
nawewe unajua kama ulivyoniimba mimi mpole, sinaga maneno ( ila kwenye
kazi ndio nakuwa mkali kama pilipili ). Ila ungetumia busara kidogo.
Just move ON kiroho safi. Naomba pia nitumie fursa hii kukupongeza
kwa tuzo yako ya MTV ila@babutale hata wewe ndugu yangu? Is this how
tunaendeleza so called uzalendo?
Inshallah Kheri lakini yote maisha wanyonge sisi iko siku Mungu atatunyanyua.
No comments:
Post a Comment