26 June 2015

Mbunge Sugu Atoa Chozi Bungeni..Adai Suala la Mtoto wake na Faiza Ally ni la Kifamilia..Adai Bado Hajamchukua Mtoto Kutoka Kwa Faiza

Jana Katika Bunge Huko Dodoma Mheshimiwa Mbunge Mlata Alisemama Haya:

"Tuna Mbunge mwenzetu amemnyanyasa mwanamke mwenzetu ametumia siku moja Mahakamani kumnyang’anya mtoto wa miaka miwili.. Mbunge huyu anajijua kwa sababu mwanamke huyo anaitwa Faiza.. Faiza arudishiwe mtoto wake"

Sugu leo amesimama Bungeni na kulitokea Ufafanuzi swala hilo na Mahakama kumpa haki ya kumlea mtoto kutoka kwa Mama yake Mzazi Faiza Ally..
Sugu Amedai yeye alipeleka vielelezo vyote mahakamani kama inavyotakiwa ambavyo ni pamoja na zile picha zilizozagaa mitandaoni zikionyesha mavazi yasio na maadili ambayo alivaa Faiza na Mwisho mahakama kuridhika kuwa kweli na Kumpa Haki ya Kumlea Mtoto..

Sugu Akaendelea kudai kuwa Swala hilo ni la Kifaragha na kifamilia zaidi na ameomba Bunge na Watu wengine kutoendelea kulijadili zaidi...

Sugu Amesema japo mahakama imempa haki ya kumchukua mtoto lakini bado mpaka sasa hajamchukua kupisha majadiliano ya kifamilia zaidi ili kuone hilo tatizo linatatuliwaje...

Mwisho Sugu alipomaliza Kuongea Alionekana Akitokwa na Machozi Usoni Mwake...

Je una Ushauri Gani kwa Sugu

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname