Baada
ya kula viapo vya kutozikana, wasanii wawili wa filamu Bongo, Wema
Isaac Sepetu ‘Madam’ na Aunt Ezekiel Grayson wamejikuta wakiangua vilio
wakati wakipatanishwa na rafiki yao mkubwa ambaye ni pedeshee
anayejulikana kwa jina la Daudi Mambya.
Aunt Ezekiel akimbembeleza Wema baada ya kupatanishwa.
Habari
kutoka kwa shuhuda wetu zilieleza kwamba, tukio hilo lilijiri wikiendi
iliyopita kwenye Ufukwe wa Coco jijini Dar ambapo Daudi aliwaita kwa
mwaliko wa mishikaki bila wenyewe kujua kinachoendelea.
Habari
zilieleza kuwa, Daudi ambaye kwake huwa hawafurukuti, amekuwa akiumizwa
mno na tofauti ya wasanii hao kwa sababu ni watu walikuwa wakipendana
hivyo kugombana kwao kulikuwa kunaleta shida kwa marafiki zao wengine.
Imefahamika
kwamba, Daudi alitumia ujanja wa kuzungumza na kila mmoja kwa wakati
wake ambapo alibaini kuwa hakuna aliyekuwa tayari kupatana na mwenzake.
Ilisemekana kuwa, Daudi alitumia ujanja wa kitaalamu ili kila mmoja kumuweka sawa bila kujijua.
“Unajua
Daudi ni rafiki yao sana, sasa hakuwa anapendezwa na tatizo ambalo
limejitokeza hivyo alitumia njia tofauti ili kuweza kuwakutanisha pamoja
tena waweze kupatana,” alieleza mtoa habari huyo.
Wakiwa na rafiki yao Daudi Mambya anayedaiwa kuwapatanishwa.
Ilielezwa
kwamba Daudi alianza kwa kumtafuta Wema na kumpeleka Coco Beach
akimuambia kuwa anataka akamnunulie mishikaki huku wakati huohuo
akimwambia Aunt naye wakutane ufukweni hapo.Shushushu wetu alizidi
kufunguka kuwa Daudi alitangulia Coco na Wema, huku akifanya mawasiliano
na Aunt na baada ya muda, Aunt naye aliwasili huku kila mmoja akibaki
katika mshangao usioelezeka baada ya kukutana uso kwa uso.
Sosi
huyo alisema kuwa Wema na Aunt walipoonana kila mmoja alikuwa kimya
lakini Daudi aliamua kuwasomea risala ndefu iliyomwingia kila
mmoja.Mambo yakipokaa vizuri, wawili hao walishuhudiwa wakiwa
wamekumbatiana huku kila mmoja akiangua kilio kilichochukua takribani
nusu saa hivyo kufanya eneo hilo kuwa kama kuna msiba.
“Yaani mpaka Daudi mwenyewe alidondosha machozi baada ya Wema na Aunt kukumbatiana na kuanza kulia.
“Yaani
ilikuwa simanzi kubwa sana,” alimalizia shuhuda huyo.Akizungumza na
gazeti hili, Daudi alisema kuwa aliamua kuwapatanisha wawili hao kwa
kuwa alikuwa hapendezwi na tatizo hilo na kwamba wote ni rafiki zake.
Kwa upande wake, Aunt alifunguka ya moyoni:
“Tulipokutana kila mtu alijua tatizo lake na tukaona ni mambo ya kijinga, ikabidi tuweke tofauti pembeni maisha yaendelee.”
Wema
alisema: “Mambo ya kugombanagombana hayana msingi na kwa vile ni mtu
mzima (Daudi) aliwakutanisha, nikaona yaishe.”Wema na Aunt ambao
walikuwa marafiki wakubwa waliingia kwenye mgogoro hivi karibuni baada
ya Wema kumtuhumu Aunt kuunga mkono shoo ya Zari All White Party ya
mwanadada Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’ ambaye ni mpenzi wa aliyekuwa
mpenzi wa Wema, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
No comments:
Post a Comment