Zuwena Mohamed ‘Shilole’.
BAADA ya wiki kadhaa
kupita tangu picha zake zisambae zikimuonesha gauni likiwa limevuka
nakuachia ‘nido’ wazi, staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’
ameibuka na kuwaomba radhi kinamama wote.
Akipiga stori na Over
The Weekend, Shilole alisema kuwa anajua kwamba kitendo hicho
kimewakwaza wengi na hakukusudia kufanya jambo kama lile. “Nimejifunza
mengi na naendelea tena kuomba msamaha kuwa tatizo hili halitajitokeza
tena ,niwaombe radhi kina mama na mashabiki wangu,” alisema. Shilole
alifanya tukio hilo alipokuwa jijini Antwepen, Ubelgiji kwenye shoo
ambapo aliongozana na mpenzi wake,Nuh Mziwanda.
No comments:
Post a Comment