Na. Richard Bakana, Dar es salaam
0656-407-587.
0656-407-587.
Katika kuanza na kumalizia siku
ya Jumapili ya Mei 2 (Jana) Dunia nzima ilisimama kwa muda kwa wapenda
masumbwi ambapo kulikuwa na mpambano wa Kihistoria kati ya Floyd
Mayweather kutoka nchini Marekani na Manny Pacquiao wa Uphillipino na
mtanange huo kumalizika Mamrekani huyo kuibuka na ubingwa kwa pointi.
Shaffihdauda.com imepita
Mtaani na kuachwa mdomo wazi na mashabiki ambao wengi wao wamempatia
Ubingwa Pacquiao wakisema kuwa ndiye aliyestahili kwani alipiga ngumi
nyingi, alishambulia mwanzo mwisho, huku wengine wakisema kuwa
Mayweather alikuwa akikimbia na hakuonyesha mchezo wa kuvutia licha ya
kushinda.
Abdul Juma mkazi wa Tegeta,
amefunguka na kusema hivi “Mchezo nimeushuhudia toka mwanzo kwenye
mapambano ya utangulizi maana sikulala kabisa nikisubiria kwa hamu
kubwa, Kama mimi ningekuwa Refa au Jaji katika mpambano huo basi
Pacquiao ndio angekuwa bingwa wangu, Kwanza alikuwa anajiamini vya
kutosha, alionyesha mchezo kweli ambao mashabiki tulitegemea maana
alikuwa anashambuli na kumuandama Mayweather muda wote, Kiukweli jamaa
alitoa burudani nzuri sana na nilitoka ukumbini nikifurahia namna
Pacquiao alivyokuwa anacheza, Mimi nadhani Pacquiao amenyimwa ubingwa
kwasababu alikuwa ugenini, majaji wote walimpendelea mwenyeji tu, Bingwa
wangu ni Pacquiao”
John Raphael wa Magomeni amesema
kuwa “Ule usemi wa mcheza kwao hutunzwa jana ndio nilikubali unafanya
kazi, Pacquiao am,ezurumiwa haki yake masikini, Hatakama majaji
wamempatia Mayweather ambaye alikuwa anakimbia ulingoni mimi nasema
Bingwa ni Pacquiao, Sawa wanasema kuwa Mayweather alikuwa anapiga ngumi
za uhakika lakini Mphillipino anajua kupiga ngumi”.
Zainabu Juma amesema “Kwanza
sikulala kabisa nikijua mpambano utakuwa saa kumi, Kam uamuzi ungekuwa
unatolewa na mashabiki basi Mayweather asingekuwa bingwa kwa Ukumbi
mzima ulikuwa unamshangilia Pacquiao kutokana na kasi aliyokuwa nayo ya
kupiga ngumi nyingi, pia alimuandama sana mpinzani wake, Lakini sisi ni
watazamaji tu Majaji wao ndio walikuwa wanajua ngumi sahihi inatakiwa
ipigwe wapi ili kupata pointi ndio maana mwisho wa siku Mmarekani
kaibuka Mshindi”
Mussa Ally ‘M’babe’ amesema
“Kwanza kabisa hawajamaa wote wanajua kupiga ngumi, Pacquiao anakasi
kubwa sana na alipokuwa akimfikia mpinzani wake alikuwa anapiga ngumi
nyingi kitu ambacho mashabiki wengi walikuwa wanafurahia lakini mwenzake
alikuwa anazikinga kwa kuficha uso ambao ndio sehemu yenye pointi, Ni
kweli kutokana na namna Pacquiao alivyocheza toka mwanzo alistahili
kushinda lakini majaji ndio walikuwa wanajua kitu sahihi, Mayweather
sawa alikuwa anaonekana kumkimbia mpinzani wake lakini hiyo yote ilikuwa
kujihami na kujilinda ambapo hapo hapo alikuwa akipata mwanya anapinga
ngumi yenye uhakika na pointi”
Hawadhi Nasibbu “Toka lini kuku
akawika ugenini bwana, Mayweather alishinda sababu yuko Nyumbani, hata
waliokuwa wakimshangilia ni watu wake wa karibu, lakini ile mashine
Pacquiao ilikuwa ikishangiliwa na kila mtu kutoka na uwezo wake na kasi
na namna alivyokuwa akimkimbiza mpinzani wake”
James Laurent “Mayweather ndio
bingwa hayo ni maneno tu ya watu, kwanza alikuwa anapiga ngumi kwa
malengo sio sawa na Pacquiao ambaye alikuwa anajipigia tu bila kujua
wapi ngumi inatakiwa kwenda,
Katika mchezo huo ulikuwa wa
kuvutia na wakihistoria uliamuliwa na majaji ambapo walimpatia
Mayweather ushindi wa pointi 116-112, 116-112, na 18-110 dhidi ya
Pacquiao.
No comments:
Post a Comment