Mbali na madai hayo,
naye baba mzazi wa Peace, mzee Sylvester Katoto (72) ameibukia jijini
hapa na kumtaka askofu huyo kujitokeza hadharani na kuikana damu yake
hiyo mbele yake.Akizungumza hivi karibuni na gazeti hili jijini hapa,
mzee Katoto alisema ameamua kufika Arusha akitokea Karagwe kumsaidia
binti yake huyo na kuongeza kwamba amesikitishwa sana kwa taarifa kuwa
Askofu Bagonza amewatelekeza watoto wake.
“Nimeamua kuyasema haya
ili jamii ijue. Bagonza aliwahi kuja kwangu (Karagwe) baada ya Peace
kujifungua mtoto wake wa kike na kunieleza kuwa, yeye ndiye mhusika wa
mtoto huyo na aliniomba nimtunzie siri kutokana na wadhifa alionao
kikanisa.
“Ninachotaka Bagonza
ajitokeze ana kwa ana na ayakane hayo maneno aliyoniambia, pia nataka
aikane damu ya hawa watoto hapa hadharani,’’ alisema.Mzee huyo aliongeza
kusema kwamba, yeye na watoto wake watatu wa kiume waliamua kufunga
safari mpaka Arusha kukanusha barua iliyoandikwa na mtoto wake (jina
tunalo) ikisema kwamba, ukoo umemtenga Peace kufuatia sakata lake na
askofu huyo kurindima kwenye vyombo vya habari.“Tutakwenda Ustawi wa
Jamii kupeleka malalamiko yetu ili waone uwezekano wa kumwita askofu.
Nimejaribu kumpigia simu na kumtumia ujumbe wa maneno (SMS) lakini
hajanijibu hadi sasa.“Lengo letu ni kuhakikisha Peace anapata haki yake
na si vinginevyo, pia namtaka askofu kuacha kuwatumia watu wengine
katika suala hili ila ajitokeze ili azungumze na mimi,’’ alisema mzee
Katoto.
Katika hatua nyingine,
Peace ambaye ndiye mlalamikaji alimtaka mtu aliyenukuliwa na gazeti moja
la kila wiki (si la Global Publishers ambayo ni makini) akidai watoto
hao ni wake, ajitokeze hadharani na awe tayari kwenda kupima kipimo cha
vinasaba (D.N.A) ili kubaini ukweli.
“Pia namtaka Askofu
Bagonza twende wote tukapime kipimo hicho kitakachothibitisha kuwa
watoto hawa baba yao ni yupi na nasisitiza askofu ajitokeze hadharani
aikane damu yake kama anaweza,” alisema Peace.Peace alikwenda mbele
zaidi kwa kusema kuwa, wiki iliyopita askofu mmoja wa kanisa hilo mkoani
Kagera (jina tunalo) alimfuata Arusha kwa ajili ya kushughulikia suala
hilo.
Alisema askofu huyo
alimwambia asiendelee tena kulitangaza jambo hilo kwani linashughulikiwa
hatua ambayo Peace alisema hadi sasa hajapata mwafaka badala yake
ameona kwenye gazeti moja la wiki kuwa aliyezaa na Peace ni mwanaume
mwingine ambaye alidai hamfahamu na kudai kwamba amepandikizwa ili
kuiaminisha jamii.
Peace kwa sasa
anajipanga kulifikisha suala hilo Ustawi wa Jamii na Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu kwa ajili ya msaada zaidi na ameiomba jamii na taasisi
zinazotetea haki ya mwanamke zijitokeze kumsaidia ili haki ipatikane.
Alimlaumu kaka yake
mmoja kwa kitendo chake cha kumvamia na kumpiga baba yake na ndugu zake
hapo nyumbani kwake baada ya kukataa ushawishi wake kuhusu kuegemea
upande wa askofu.
Gazeti hili lilimtafuta
Askofu Bagonza kwa njia ya simu ambapo alipokea na baada ya mwandishi
kijitambulisha alikata simu na alipopigiwa tena alipokea mtu
aliyejitambulisha kuwa ni dereva wake ambaye alisema askofu alikuwa
bize.
Katika Gazeti la Ijumaa
Wikienda (ndugu na hili), toleo la 407, Aprili 20-26, 2015, ukurasa wake
wa mbele kulikuwa na habari yenye kichwa; AIBU…ASKOFU KKKT APIGA MIMBA
MBILI NJE YA NDOA.
Katika habari hiyo,
Peace alimlalamikia askofu huyo kwa kumzalisha watoto wawili, Piana (6)
na Bariki (3) lakini amewatelekeza.Alisema kufuatia hali hiyo,
alimfungulia askofu mashitaka katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha
na kunukuliwa katika jalada lenye kumbukumbu Na. AR/RB/5290/2015
KUTELEKEZA FAMILIA
No comments:
Post a Comment