22 May 2015

MAMA ASAULA NGUO ZOTE KUMLAANI SERENGETI BOY WAKE JIJINI DAR!


Heeh! Makubwa! Mama mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amefanya aibu ya mwaka baada ya kusaula (kuvua) nguo zake na kubaki mtupu, kisa kikidaiwa ni kumlaani ‘serengeti boy’ wake aliyemfanyia kitu mbaya. Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo mbali ya kuwa na mtu wake amedaiwa kuwa na tabia ya kuchepuka na wanaume tofauti ambapo amekuwa akifanya hivyo kwa kupanga chumba katika moja ya gesti (jina kapuni) iliyopo Sinza kwa Remmy, jijini Dar. Inadaiwa kuwa tukio hilo lililotokea hivi karibuni, mwanamke huyo kama kawaida yake alipata mteja ambaye ni mdogo kwake kiumri, ambaye pia ni mkazi wa eneo kulikotokea varangati hilo.
“Walikubaliana na huyo kijana kupumzika kwa muda na yule mwanamke katika chumba alichopanga, baada ya kumaliza mambo yao kijana aligoma kumpa hela ndipo mtiti ulipoanzia,” kilimwaga ubuyu chanzo chetu.  

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname