22 May 2015

John Bocco afichua siri ya Taifa Stars kuvurunda, ataja sababu kibao!


thumb_IMG_1350_1024
Nikiwa kama mchezaji waki TANZANIA ninaecheza ligi ya hapa nyumbani na nikiwa mmoja wa wachezaji katika Timu ya Taifa ya kizazi hiki cha sasa wa Mudamrefu. Naandika hivi nikiwa na huzuni na masikitiko makubwa juu ya mpira wetu wa TANZANIA kwa ujumla kuanzia club zetu, ligi yetu na mpaka kwenye Timu ya TAIFA ‘TAIFA STARS’.
Sijaandika ivi kwania ya kufundisha wala kukosoa MSHABIKI, KIONGOZI WA MPIRA, VILABU VYA TANZANIA, SHIRIKISHO LA MPIRA WA TANZANIA na wala TIMU YETU YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU. Toka nilipopata akili ya kuutambua mpira wa TANZANIA
kwakuusikiliza kwenye redio na pia kuona bahazi ya mechi kwenye Tv za vilabu pamoja na Timu ya TAIFA nilikuta ukiwa na lawama upande wa Wachezaji pamoja na Uongozi wa uendeshaji wa mpira wa VILABU pamoja na TIMU YA TAIFA mpaka nilisikia timu yetu ya TAIFA IKIITWA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU. Mimi nikiwa kama Mtanzania pia nikiwa miongoni mwanafamilia ya mpira wa tanzania pia inaniuma sana nikiiona mioyo ya watanzania wa penda soka mamilioni ikiteseka kutopata furaha ya mpira.
Wewe kama mtanzania mpenda soka, Unahisi furaha inakoseshwa na Wachezaji wa kitanzania, Uongozi na uendeshaji mpira wa kitanzani, Mashabiki wa kitanzania au TATIZO NI NINI?????????
Kwafikra zangu mimi nahisi mpira wa tanzania unaasiriwa 1. Kutokuwa na program za kuendesha mpira kisasa 2. Kutokuwa na misingi endelevu ya kuendesha wachezaji wa dogo kisasa 3.kutokua na ligi kuu bora nchini 4.Kuwa na huaba wa wachezaji wachache wanachezesha njee ya nchi ndani ya Timu ya TAIFA 5.Kutothamini na kueshimu wachezaji wakitanzania walio ndani ya ligi yetu na njee ya ligi yetu etc.
1. PROGRAM ZA KISASA ZA KUENDESHA MPIRA WETU.
Tanzania tupo nyuma sana yani tunaongoza mpira kizamani sana kwa upeo wangu mimi wa sasa mpira hauchezwi na kipaji tu Bali pamoja na elimu ya mpira Ndio manawenzetu wanakuwa na shule za mpira, mfano’ sisi watanzania tunaleta makocha wa kisasa kwenye club zetu pamoja na timu yetu ya taifa, ila mnasahau kuwa wachezaji wenu hawajaandaliwa kisasa pia hata makocha wanaowafundisha sio wa kisasa. Tunatakiwa sasa tuamke kuwapeleka makocha wetu wakajue mpira wakisasa unavofundishwa ili waje kuwafundisha wachezaji mpira huo ili hata tukileta makocha wakigeni ambao ni wakisasa wawe wanatuongezea kipya sio kuanza tena moja. Pia na shirikisho la mpira liongoze mpira kisasa hata kwakuiga basi nchi zilizoendelea zaidi yetu kimiprira kuwa walianzaje na wamewezaje sio kwa mifumo yetu hii yakizamani na mawazo yetu ya mtu mmoja mmoja.
2. KUTOKUWA NA MISINGI ENDELEVU YA KUENDESHA WACHEZAJI WA DOGO KISASA.
Tanzania tunauhaba wa vituo vya kuendesha soka na kutengeneza vipaji vya vijana wadogo pia tuna utamaduni ambao sio wakisasa wa kuinua na kutengeneza vipaji hapa nchini, sisi watanzania club na shirikisho letu huwa wanainua vipaji sio kutengeneza vipaji kama kwa nchi za wenzetu. Kutengeneza kipaji ni nini ?? Kutengeneza kipaji katika soka nikumchukua Mtoto asiejua hata maana ya kupiga pasi, krosi shuti na kuanza kumfundisha moja baada ya moja mpaka kufikia kugeuka na mpira na kupiga chenga. Kuinua kipaji ni nini?? Kuinua kipaji nikumkuta Mtoto wa umri wamiaka 15,16 mpaka 17 na kuendelea akiwa anajua nn maana ya kupiga pasi,krosi,kugeuka na mpira na mpaka kupiga chenga, kwamaana hiyo sasa ukifatilia club zetu hata shirikisho letu la mpira hawana malengo na watoto wenye umri wa miaka 8,9,10,11,12,13,14 na 15 kuwaandaa ambao hawa unaweza kuwapa msingi wowote wa soka unaoutaka Bali tunaanza na watoto wa umri wa miaka 17,18,19 na 20 na kuendelea ambao washapitia kwenye misingi ya kizamani ambayo yamitaani ya kupiga pasi,krosi na chenga, ambao umri huo nchi za wenzetu zilizo endelea umri huo wa miaka 17…..20 unawakuta wakiwa tayari na wekicheza Timu kubwa pamoja na timu ya taifa kwa mafanikio sio kwakupata uzoefu. Tuamke watanzania pamoja na shirikisho letu na vilabu vyetu tusitake mafanikio ya haraka ambayo yanazidi kutupotezea muda kumchukua mchezaji wa umri wa miaka 17 nakuendelea aliepitia misingi mibovu ya mpira ndio ukataka umbadilishe na kocha wa kisasa wakigeni wa u17 wa timu ya taifa bali tuchukue Mtoto wa miaka 8..mpaka..12 tumpe kocha wa kisasa, madocta wakisasa, elimu ya kisasa na malezi ya soka la kisasa alfu tuone kama hatutoweza shiriki kombe la Africa.
3. KUTOKUWA NA LIGIKUU BORA NCHINI.
kuwa na ligikuu bora chini nikioo kwa kuinua mpira wa nchi yetu, kwa mfano kama kwa sisi tanzania naweza kusema asilimia 90% ya wachezaji wa Timu ya taifa wanatoka katika ligi yetu ya nyumbani lakini kiukweli ligi yetu haina ubora kuanzia kwa maandalizi ya wachezaji toka walipoanzia soka (mafunzo ya soka waliyoyapata) pili uendeshaji wa club zetu hapa nchini miundombinu inayotumiwa kuendesha ligi yetu hapa nchini mfano viwanja tunavotumia vibovu, mipira tunayotumia mibovyu kwenye ligi jezi mbovu waamuzi sio wazuri ni waamuzi wanachezesha kizamani, kwasababu tukija kucheza mechi zakimataifa tunakutana na mipira mizuri viwanja vizuri waamuzi wazuri wakisasa na ndio mana timu za tanzania kwenye mashinda ya kimataifa tunapata kadi nyingi ofsaidi nyingi mwisho tunafungwa kumbe tatizo tulizoeshwa vibaya na marefa wa ligi yetu. Kwamaana iyo basi huwezi kumpata mchezaji wa Timu ya taifa mzuri kutoka kwenyeligi yetu mbovu isiyo na viwanja bora mipira bora uongozi bora marefa bora wala mashabiki bora, hiyo nichangamoto kwetu watanzania wote wapenda soka tushtuke na tubadilike ili mpira wetu uinuke bilaivo mtalaumu wachezaji tu mpaka Somalia watashiriki world cup sisi hata Afican cup hatutagusa.
Waandishi wa habari na mashabiki wa MPIRA WA TANZANIA muamke na mbadilike kunavitu muhimu sana vya kusema ili soka la tanzania libadilike kunavitu Vingi sana vya kusema ili vibadilishwe ili tanzania tusiwe tena vipofu kwenye ulimwengu huu wa soka la kisasa sio soka la mdomoni wala magazetini sio soka lakupanga Timu ya TAIFA kwenye gazeti au kwenye vijiwe jioni tukikaa ila imefikia wakati wa kupanga timu au kuchagua timu kwa mtu husika sio kwamawazo ya mtu mmoja mmoja, kwakufanya mabadiliko ya kuwa na ligi bora ili tupate wachezaji bora kwa ubora wao utatengeneza Timu ya taifa bora na tutapata wachezaji wengi watakao fikia kiwango chakucheza mpaka njee ya nchi ambao tukifikia hatua hiyo tutakua na Timu ya TAIFA bora zaidi kwa badae ambayo tukija kupangwa tena na NIGERIA miaka ya badae tutakua na uwakika wakuwafunga ila kwa hivi tunavoenda hatatukiwafunga tumewabahatisha tu kiukweli TANZANIA tulipo sasa na soka la ulimwenguhuu lilivofikia bado sana. Tubadilikeni watanzania hii niaibu si kwa wachezaji tu ila ni kwanchi nzima mtawalaumu wachezaji tu ila wachezaji sio tatizo tatizo tunamifumo ya kizamani alafu bado tunailazimisha iendelee.
TULISHAFELI..TUMEFELI..NA TUSIPOAMKA TUTAFELI KABISA yani tutakua wa mwisho KABISA duniani. Ebu jiulize wewe mwenyewe uliviona vizazi vingapi tanzania vilivyopita na vilikua na wachezaji wazuri????? Ukipata jibu jiulize tena vilietea mafanikiogani kwenye timu ya taifa au vilabu vyetu ambayo tunajivunia sasa???? Kwa mimi toka nivisikie na kuadisiwa mpaka leo nacheza sijao mafanikio zaidi ya kuwa na sifa zisizofaidisha nchi. Tubadilikeni jamani hayo nimawazo yangu tu kama nimewakosea nisameeni ila hata sisi wachezaji mnaotutukana mais kutuona sio wazalendo inatuumapia kwasababu tunatumia nguvu zetu bilamafanikio nakinachouma zaidi hatupendi kufeli ila tunafelishwa inauma kwa kweli ila nyumbani ni nyumbani TUNAIPENDA NCHI YETU NA TUTAIPENDA MILELE ila tusikubali kupelekwa tubadilikeni watanzania
Makala hii imeandikwa na nahodha wa Taifa Stars kwenye michuano ya Cosafa, John Raphael Bocco

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname