Staa anayevuna fedha
nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’
amewatelekeza watoto katika Shule ya East Africa International jijini
Dar ambao aliahidi kuwalipia ada, Risasi Mchanganyiko linakuwa la kwanza
kukudondoshea.
Wanafunzi wanaodaiwa kutelekezwa na Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Chanzo makini
kililiambia gazeti hili juzi kwamba, baada ya Diamond kuwashindanisha
watoto hao, Hillary na Hamis (katika picha no. 1 na 2 zilizoko ukurasa
wa mbele walipelekwa shule na Diamond) katika shindano la Ngololo
lililonyika Januari, mwaka jana katika Viwanja vya Leaders Club, Dar na
kushinda aliamua kuwapeleka katika shule hiyo na kuahidi kuwalipia ada
kila mwaka lakini kuanzia hapo aliwatelekeza.
“Jamani Diamond kila
kukicha anafanya shoo za mamilioni lakini ameshindwa kuwalipia ada wale
watoto ambao aliahidi kuwasomesha. Wamesoma mwaka mmoja tu, mwezi
uliopita walitimuliwa na sasa wako nyumbani. Inauma sana kwani hawa
watoto walitolewa kwenye shule za kawaida na yeye ndiyo akawapeleka
kule,” kilisema chanzo hicho.
WAZAZI WANASEMAJE?
Akizungumza na gazeti
hili, mmoja wa wazazi wa wanafunzi hao, Fadhili alisema watoto wao
walitimuliwa shuleni tangu April mwaka huu kwa kuwa, Diamond hakuwahi
kuwalipia ada tangu alipowaingiza pale.“Inauma sana, kwani tangu watoto
wetu watimuliwe tumekuwa tukifuatilia kwa mtu tuliyeambiwa ni msimamizi
wa Diamond (jina lake linahifadhiwa kwa sasa) lakini hatupi jibu la
kueleweka.
Nasibu Abdul ‘Diamond akiwa na wanafunzi hao pamoja na mwalimu wao.
“Tulipewa namba za simu
za mameneja wa Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ na Said Fella lakini
kila tukiwapigia simu tunaambiwa msanii huyo hayupo Dar, mara amesafiri,
mara yuko kwenye shoo, yaani kila siku tunazunguka tu hatujui tufanye
nini.
“Tunaomba sana jamani,
mtusaidie na nyie waandishi maana watoto wanapitwa na masomo na isitoshe
kabla ya hapo walikuwa wakisoma kwenye shule za kawaida,” alisema mzazi
huyo.
MSIKIE MWALIMU MKUU
Paparazi wetu alifunga
safari mpaka shuleni hapo maeneo ya Mikocheni, Dar na kufanikiwa
kuzungumza na Mwalimu Mkuu, Mercy Githirua ambapo alithibitisha watoto
hao kusimamishwa masomo kutokana na kukosa ada.“Tulivumilia kwa muda
mrefu sana kwani tulimwamini Diamond tukawapokea watoto hao na kuanza
masomo. Siku aliyokuja kuwakabidhi hapa shuleni aliomba ‘invoice’ kwa
ajili ya kututumia ada lakini yuko kimya mpaka leo.
...Akisalimiana na mwalimu.
“Hata fedha ya
kuwashonea sare za shule ilibidi niwasiliane na (linatajwa jina,
linasitiriwa) maana tunafanya naye kazi nyingi, akatoa hizo fedha lakini
ada ndiyo ikawa tatizo. Hivyo ilipofika Aprili 14, mwaka huu ilibidi
niwarudishe nyumbani mpaka kieleweke kwa kweli.
“Sijapenda tabia ya
Diamond, hivi anajua watoto wakimchukia itakuwa ni hatari sana kwake?
Watoto wa watu walikuwa wanasoma huko akaenda kuwatoa na kuwaleta hapa
lakini amewatelekeza, siyo vizuri kabisa,” alisema mwalimu mkuu huyo.
WANADAIWA SHILINGI NGAPI?
Kwa mujibu wa mwalimu
mkuu huyo, watoto hao tangu walivyoingia Januari 21, 2014 hawakuwahi
kulipiwa ada yoyote hivyo kila mmoja anadaiwa shilingi milioni moja na
laki sita (1,600,000).
Staa anayevuna fedha nyingi kupitia kipaji chake cha muziki, Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
DIAMOND, MAMENEJA WAKE!
Juzi, gazeti hili
lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond kwa njia ya simu lakini ilikuwa
imesetiwa kwamba inafanya kazi muda wote ‘bize’ hata alipotumiwa meseji
hakujibu. Vivyo hivyo kwa mameneja wake, Fella na Bab Tale simu zao
ziliita bila kupokelewa.
TUJIKUMBUSHE
Mwaka jana, Diamond
aliandaa shindano la Nani Anaweza Kucheza Staili ya Wimbo wa Ngololo
ambapo watoto kibao walijitokeza Leaders Club. Watoto hao wawili
waliibuka kidedea kwa kuonesha uwezo mkubwa wa kucheza na ndipo zawadi
yao aliamua kuwapeleka kwenye shule hiyo na kukutwa na yaliyowakuta!
No comments:
Post a Comment