24 April 2015

MSANII WA BONGO MOVIES, KUPA ANASWA NA MWANAUME TATA

Na Richard Bukos
Msanii wa filamu mwenye vituko kibao, Idrisa Makupa ‘Kupa’ juzikati aliwaacha watu midomo wazi baada ya kunaswa akiwa beneti na mwanaume tata maarufu mjini anayefahamika kwa jina la Danny.Wawili hao walibambwa na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Escape One uliopo Mikocheni jijini Dar kulikokuwa na onesho la mwanamuziki Christian Bella.


Msanii wa filamu mwenye vituko kibao, Idrisa Makupa ‘Kupa’ akiwa na mwanaume tata huyo.
Gumzo lilianza pale Danny alipomsogelea Kupa na kumnong’oneza, jambo lililowafanya watu wahoji ukaribu wa kijana huyo na msanii huyo unakujaje!Hata hivyo, wawili hao baada ya kuona wanapigwa sana picha ‘walimtoka’ paparazi wetu hadi walipokuja kunaswa tena baadaye wakiwa wamegandana, hali iliyotafsiriwa tofauti.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname